Mhe. Mbunge wa jimbo la Urambo-Tabora ( Mama Magret Sitta) wa pili kushoto akikabidhi mchango wa mabati 128 katika shule ya msingi shikizi ya Kangeme iliyoko kijiji cha Izimbili kata ya Uyumbu. Aidha Jumla ya mabati 1068 yaliyotolewa na Halmashauri ikishirikana na wadau mbalimbali ikiwemo PSPF, NMB, Wafugaji wa Wilaya ya Urambo, Wananchi, na Watumishi wa Halmashsuri ya Wilaya ya Urambo.
Bati hizi ziligawika katika shule za msingi 18 zilizokuwa na upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa.
Mkurugenzi Mtendaji(W) URAMBO Bi Margaret Jonathan Nakainga anawashuru wadau wote wa Elimu waliojitoa katika kufanikisha zoezi hilo na anaomba wadau wengine wenye mapenzi mema na maendeleo katika wilaya ya Urambo wajitokeze ili kuondoa changamoto za Elimu.
Bomani Urambo
Anunani ya posta: S.L.P 170
Simu ya mezani: 07322988305
Simu ya mkononi: 0769532059
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Hatimiliki © 2018 Urambo. Haki zote zimezingatiwa