• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Urambo  District  Council
Urambo  District  Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za mitaa Halmashauri ya wilaya ya Urambo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Elimu msingi
      • Elimu sekondari
      • Idara ya Mazingira
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Ufugaji Nyuki
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
    • Kata
      • Kata Zetu
    • Kibali cha Safari
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Watalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kiutumishi
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Afya, Elimu na Maji
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya UKIMWI
      • Kamati Nyinginezo
        • Kamati ya Ugawaji wa Viwanja
        • Kamati ya Ajira
        • Kamati ya ALAT Mkoa
        • Wajumbe wa Mamlaka ya Mji Mdogo
    • Ratiba ya Vikao
    • Taarifa mbalimbali
  • Miradi
    • Miradi Mipya Itayotekelezwa
    • Miradi inayaoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
    • Sheria
    • Taarifa
    • Taratibu
    • Zabuni
  • Kituo cha Habari
    • Picha
    • Hotuba
    • Matukio
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video

Naibu Waziri Mgalu Apiga Goti Kuwashukuru Wananchi Urambo

Siku iliyowekwa: July 18th, 2019


Na. Edward C.Rumanyika, Urambo

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu amepiga goti kama ishara ya kuwashukuru wananchi wa Kijiji cha Uhuru, Kata ya Vumilia Wilayani Urambo mkoani Tabora, baada ya wananchi hao kutoa eneo la ekari tano bure kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha kupoozea umeme.

Naibu Waziri Mgalu alitoa shukrani hizo kwa wananchi Jumatano Julai 17, 2019 na kuupongeza uongozi wa Kijiji cha Uhuru na kueleza kuwa kukamilika kwa ujenzi kituo cha kupoza umeme kitakachojengwa katika eneo walilolitoa ifikapo mwezi Agosti mwaka 2020, kutaondoa adha ya kukatika kwa umeme katika Wilaya za Urambo, Uyui na Kaliua.

"Wananchi wa kijiji cha Uhuru mmekuwa watu wa pekee kwa kutoa ardhi yenu kutuwezesha kujenga kituo hiki bila ya kudai fidia, na sisi  Serikali ya Awamu ya Tano tunatambua mchango wenu mkubwa tunapoelekea katika uchumi wa viwanda hivyo nasema ahsenteni," aliwashukuru wananchi huku akiwa amepiga magoti mbele ya umati wa wananchi.

Awali akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huo ,Mhandisi wa Mradi huo Julius Kabengwe, alisema kuwa mradi utagharimu shilingi 1, 160,429,066 kwa awamu ya kwanza na mradi utatekeleza  kazi za ujenzi wa uzio, ofisi za kuendeshea kituo, barabara ya kuingia kituoni toka barabara ya Urambo-Kaliua, ununuzi na ufungaji wa transifoma kubwa mbili zenye uwezo wa 10 MVA kila moja na ujenzi wa laini ya msongo wa kilovoti 132kV kutoka Tabora mjini hadi Uhuru-Urambo.

Katika hatua nyingine, Mhe. Mgalu alizindua umeme wa mradi wa REA Awamu ya III Mzunguko wa Kwanza-Urambo, wenye urefu wa kilometa mbili unaotekelezwa  katika kata ya Kasisi kijiji cha Wema.

Akihutumia wananchi, viongozi wa Serikali na Chama,  Naibu Waziri aliuagiza uongozi wa TANESCO-Urambo na REA-Urambo kuhakikisha mitaa 13 iliyoko Urambo inasambaziwa umeme na kuwafungia wananchi kwa bei isiyozidi shilingi 27,000 na kumtaka mkandarasi wa mradi wa REA awamu ya III mzunguko wa Kwanza kuhakikisha vijiji saba vilivyo salia vinasambaziwa umeme katika REA Awamu ya III mzunguko wa Pili ili kuifaya wilaya ya Urambo kuwa mingoni mwa wilaya zenye umeme kila kijiji.

Aidha, Mhe. Magalu alizisisitiza TANESCO na REA  pia kupeleka umeme katika taasisi mbalimbali zikiwemo nyumba za ibada, vituo vya umma na binafsi vya kutolea huduma na akasisitiza kuhakikisha kila nyumba inayostahili kuwekewa umeme iwekewe bila kujali kama nyumba hiyo niya udongo au tofali.

Kwa upande wake, Bi. Yulitha Misalaba ambaye nyumba yake ilifanyiwa uzinduzi kwa kuwashwa umeme, alimshukuru Naibu Waziri na Mbunge wa Urambo Mhe. Magreti Simwanza Sitta kwa juhudi zake za kuhakikisha anatimiza ahadi alizozitoa wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2015.

"Nafuhi sana kwani na sisi tutakuwa kama wa mjini, kwani tulikuwa tunahangaika sehemu za kuchajia simu zetu, yaani ahasante sana Mbunge wetu, ahasante Magufuli", alieleza kwa furaha Bi. Misalaba.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi, Diwani wa Kata ya Kasisi, Mhe. Japhet Kakumbi alielezea kufurahishwa na mradi wa REA Awamu ya III mzunguko wa Kwanza kuanzia katika Kata anayoiongoza na kuishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kazi nzuri ya kuwaletea wananchi wake maendeleo na kuwaomba wananchi kutumia umeme huo kama fulsa kwa kuanzisha biashara mbalimbali zikiwemo saluni za kike na kiume, mashine za umeme za kusaga na kukoboa nafaka na kuwataka wanafunzi watumia umeme huo kusoma na kujifunzia.

Matangazo

  • Maotokeo ya Mtihani wa Kidato cha IV, II na Darasa la nne, 2020 January 15, 2021
  • Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga Kidato Cha I, 2021 December 18, 2020
  • Kuitwa Kazini Kada ya Afya July 09, 2018
  • Matokea Kidato cha Sita na Uwalimu July 13, 2018
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Sekondari 14 Urambo Zapata Huduma ya Intaneti

    October 20, 2019
  • Naibu Waziri Mgalu Apiga Goti Kuwashukuru Wananchi Urambo

    July 18, 2019
  • Pro.Ndalichako Akata Utepe VETA-Urambo

    July 09, 2019
  • Yaliyojili Urambo siku ya Meimosi

    May 01, 2019
  • Angalia zote

Video

Waziri wa maji, Prof. Makame Mbarawa
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Tovuti ya ofisi ya mkuu wa mkoa
  • FFARS USER GUIDE
  • PlanRep DOCUMENTATION
  • Facility Financial Accounting and Reporting System (FFARS)
  • Kata Zetu
  • BEMIS
  • Wahe. Madiwani

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa
  • Tovuti ya sekretarieti ya Ajira
  • Fomu ya Maadili ya Viongozi kwa Mtandao
  • Public Service
  • Matokeo ya Mtihani wa Taifa Tanzania.
  • Ikulu

Waliotembelea Tovuti

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Sehemu

Wasiliana nasi

    Bomani Urambo

    Anunani ya posta: S.L.P 170

    Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824

    Simu ya mkononi: 0784828287

    Barua pepe: ded@urambodc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • sera ya faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2021 Urambo . All rights reserved.