Maendeleo ya Jamii
1.0 Utangulizi
Idara ya Maendeleo Jamii, na Ustawi wa Jamii ni miongoni mwa Idara 13 na vitengo 6 vinavyojitegemea katika Halmashauri ya Wilaya ya Urambo, na ni kiungo muhimu kati ya Halmashauri na jamii kwa kuratibu na kusimamia shughuli za Halmashauri.
1.1 Muundo wa Idara
Idara ina vitengo Vikuu Vitatu ambavyo ni:
1.2 Shughuli za Idara.
1.2.1 Maendeleo ya Jamii
Kushirikisha jamii katika kubaini, kubuni, kupanga, kutekeleza na kufuatilia miradi mbalimbali ya Maendeleo.
Kuongoza na kusimamia utekelezaji wa mipango/miradi ya Maendeleo.
Kufanya utafiti na kutoa mapendekezo ya namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali za maendeleo kwa kushirikiana na watumishi wa sekta nyingine.
Kuelimisha viongozi wa Serikali katika ngazi mbalimbali na viongozi wa dini na mashirika yasiyo ya kiserikali kuhusu Sera mbalimbali za Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto.
Kuelimisha na kuhamasisha jamii kupambana na VVU na UKIMWI.
Kueneza elimu ya Uraia mwema.
Kufanya uchambuzi wa matatizo ya jamii na kutoa ushauri wa kitaalamu kwa ngazi zingine.
Kuvisaidia vikundi maalum (vya ushirika, vikundi vya kijamii, vya kidini, n.k.) kuandaa miradi na kuwaelekeza namna ya kupata mitaji.
Kuelimisha jamii juu ya kutekeleza masuala ya kijinsia na kuratibu shughuli zote za Maendeleo ya Jamii kwa kuzingatia jinsia.
Kuhamasisha jamii kuondokana na mila/desturi zilizopitwa na wakati na kuwa na mtazamo wa kupenda kuleta mabadiliko.
Kuratibu shughuli za mifuko/mikopo ya wanawake.
Kuhamasisha jamii kutumia teknolojia rahisi na sahihi na.
Kuelimisha jamii kuhusu masuala ya watoto.
Kuratibu maadhimisho mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa.
1.2.2 Ustawi wa Jamii
Kusimamia utekelezaji wa Sheria, Sera, Miongozo, Kanuni na viwango vya ubora katika utoaji wa huduma mbalimbali za ustawi wa jamii.
Kufanya tathmini, ufuatiliaji na utaratibu wa huduma za ustawi wa jamii.
Kujenga uwezo wa kitaaluma kwa Maafisa Ustawi wa jamii ili waweze kutoa huduma timilifu kwa wananchi.
Kufanya tafiti zinazohusu huduma za ustawi wa jamii.
Kuwajengea uwezo watumishi wa ustawi wa jamii na Wadau katika utoaji wa huduma.
Kuanzisha na kuendeleza programu za kushawishi, kutetea na kulinda haki za makundi maalumu yakiwemo watu wenye ulemavu wa viungo na ngozi, wazee na wasiojiweza, familia zenye dhiki na watoto waishio katika mazingira hatarishi.
Kujenga Uhusiano na wadau wa nje na ndani ili kutoa huduma bora za ustawi wa jamii.
Kuratibu shughuli za mabaraza ya vijana.
1.2.3 Maendeleo ya Vijana
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2024 Urambo . All rights reserved.