5.0. HUDUMA:
Idara inatoa huduma takribani kwa jumla ya wananchi 192,781 kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 wa Wilaya ya Urambo.
5.1: Utoaji wa huduma
Idara inatoa huduma kwa siku 5 za wiki kuanzia saa 1:30 asubuhi hadi 9:30 mchana kama ifuatavyo:-
Kutoa vibali vya idhini ya kufyatua matofari katika eneo la Mamlaka ya Mji Mdogo Urambo kwa kiindi cha mwezi Machi hadi Oktoba baada ya kufanya ukaguzi wa eneo husika la vichuguu ili kudhibiti uharibifu wa mazingira.
Kugawa miche ya miti kwa wananchi mwezi Desemba hadi Aprili kila mwaka kwa ajili ya kupanda katika maeneo ya makazi, taasisi na mashamba binafsi ya miti ili kuboresha mazingira.
Kutoa ushauri (Extension services) bure juu ya uoteshaji, upandaji na utunzaji wa miti kwa siku za Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 1:30 asubuhi hadi 9:30 mchana.
Kutoa ushauri bure kwa wawekezaji wa miradi mikubwa ya kibiashara juu ya kufanya tathmini ya athari kwa mazingira kabla ya kutekeleza mradi.
Kuhakikisha huduma bora ya uzoaji taka ngumu na maji taka inatolewa kwa wakati kwa wananchi wanaokaa katika eneo la Mamlaka ya Mji Mdogo Urambo.
6.0. MAJUKUMU YA IDARA
Idara inahamasisha wananchi kutunza mazingira kwa kupanda na kutunza miti ya matumizi mbalimbali ya kuni/nishati kivuli, mbao na matunda pamoja na kutunza uoto wa asili kuboresha mazingira ya Wilaya yetu.
Idara inahamasisha na kusimamia usafi na utunzaji wa mazingira katika maeneo ya makazi, vyanzo vya maji, biashara, stendi, taasisi, vizimba vya kukusanyia taka ngumu, mashirika, viwanda, michezo, maegesho, kumbi za starehe na maeneo ya wazi.
Idara inasimamia taratibu za ukusanyaji wa taka ngumu na unyonyaji wa maji machafu kutoka katika makazi na maeneo ya shughuli za kibiashara na kupeleka katika maeneo ya dampo yaliyotengwa kwa kazi hiyo ili kudhibiti magonjwa ya mlipuko na uchafuzi wa mazingira.
Idara inatoa ushauri kwa Wananchi wanaotaka kuwekeza katika miradi mikubwa ili waweze kuzingatia Sheria ya Mazingira Na. 20 ya mwaka 2004 inayoelekeza kuzingatia taratibu za tathmini ya athari kwa mazingira kabla ya kutekeleza mradi.
7.0: MPANGO MKAKATI WA USAFI WA MAZINGIRA
SIKU ZA KAMPENI YA USAFI WA MAZINGIRA (KILA JUMAMOSI YA MWISHO YA KILA MWEZI NA KILA ALHAMISI YA KILA WIKI)
JUKUMU LA MWANANCHI AFANYE NINI?
MAJUKUMU YA MJI MDOGO URAMBO IDARA YA USAFI NA MAZINGIRA
Idara hii itashughulika na Ukusanyaji, uzoaji na utupaji wa taka ngumu.
Taka zilizopo katika mifuko/dust bin kwenye vitongoji au mitaa.
|
Taka toka katika masoko
|
Taka za stend ya mabasi
|
Kuondosha Mizoga mbalimbali katika makazi ya wananchi
|
Taka zilizopo maeneo ya wazi
|
|
Mpango kazi (Usafi wa Mji) kwa kutumia vikundi vya kijamii siku ya Jumatatu – Jumamosi.
Saa 1:30 Asubuhi – 2:00 Asubuhi – Vikundi kuandaa na kuchukua vifaa vituoni (Makwama / Guta/ Roli).
Saa 2:00 Asubuhi – 9:30 Mchana – Makwama / Maguta/Magari kupita katika vituo vya kuzolea taka na mizunguko katika vitongoji na kueleka taka dampo.
8.0. SHUGHULI MBALIMBALI ZILIZOTEKELEZWA NA IDARA
8.1. Utekelezaji wa zoezi la Upandaji Miti katika Wilaya ya Urambo
Serikali, kwa lengo la kuhakikisha kuwa mazingira ya nchi yetu yanarejeshwa katika hali ya ubora, ilitoa agizo kuwa kila Halmashauri ya Wilaya ihakikishe inazalisha na kupanda miche ya miti 1,500,000 kila mwaka.
Jedwali Na. 1: Utekelezaji wa malengo ya upandaji miti kuanzia mwaka 2010/2011 hadi 2017/2018 Wilayani Urambo.
Mwaka |
Lengo la upandaji |
Miti iliyopandwa |
Miti iliyostawi |
Ustawi (%) |
2010/2011 |
1,500,000 |
2,094,235 |
1,465,965 |
70 |
2011/2012 |
2,000,000 |
3,500,000 |
2,555,000 |
73 |
2012/2013 |
2,000,000 |
3,350,294 |
2,680,236 |
80 |
2013/2014 |
2,000,000 |
1,525,663 |
1,144,248 |
75 |
2014/2015 |
2,000,000 |
2,647,510 |
2,065,058 |
78 |
2015/2016 |
1,500,000 |
1,531,960 |
1,087,691 |
71 |
2016/2017 |
1,500,000 |
2,210,119 |
1,502,880 |
68 |
2017/2018 |
1,500,000 |
2,684,509 |
- |
- |
Jumla |
14,000,000 |
19,544,290 |
12,501,078 |
64 |
HABARI PICHA SOMA HAPA |
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.