Wednesday 22nd, January 2025
@Makao makuu ya Wilaya
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji(W) URAMBO kwa kushirikiana na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la URAMBO pamoja na ofisi za MKURABITA, wanatarajia kuzindua kituo cha ofisi za Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge (MKURABITA) hivi karibuni.
kituo hicho kitakuwa na ofisi za
|
|
|
|
|
|
|
MKURABITA ni Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania. Ni Mpango ulioanzishwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mpango huu unasimamiwa na Ofisi ya Rais – Ikulu.
Chimbuko la Mpango huu ni mwelekeo wa Sera za Chama cha Mapinduzi (CCM) miaka ya tisini katika kumilikisha uchumi kwa Watanzania ili kuwawezesha kutumia mtaji uliofichika katika rasilimali na biashara zao na hatimaye waweze kushiriki katika mchakato wa uchumi rasmi unaotawaliwa na sheria.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba Watanzania Walio wengi wanamiliki rasilimali na kuendesha ambazo hazina uhai wa kisheria katika sekta isiyo rasmi. Mtaji uliofichika katika rasilimali na biashara hizo hautambuliki. Hivyo wamiliki wake hawajumuiki kikamilifu katika uchumi rasmi. Hivyo hawanufaiki na fursa zilizopo pia hawachangii kikamilifu katika kukuza uchumi wa nchi.
Kwa hiyo urasimishaji wa rasilimali na biashara unakusudiwa kuzipa rasilimali na biashara za Watanzania walio wengi uhai wa kisheria ambao utawezesha kuwa na sifa tatu muhimu kama zifuatazo zinazowawezesha kukuza mitaji na kuongeza pato.
|
MKURABITA ni sehemu ya Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini Tanzania (MKUKUTA) na Mkakati wa Kuondoa Umasikini Zanzibar (MKUZA), ukilenga kuwawezesha walengwa kutumia rasilimali na biashara zao zilizo rasimishwa katika kujipatia mitaji, soko pana na fursa zingine zinazopatikana katika sekta rasmi na hivyo kupunguza umaskini wa kipato.
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.