Thursday 21st, November 2024
@Urambo DC headquarter
Leo Alhamisi ya tarehe 8.03.2018 wanawake wote Duniani wanasherekea tukio la mafanikio yao. Kwa Halamshauri ya Wilaya ya Urambo, wnawake wamejitokeza kusherekea siku hii huku wakiwa na kauli mbiu ya " Kuelekea Uchumi wa Viwanda, Tuimarishe usawa wa Jinsia na Uwezeshaji wa Wanawake wa Vijijini"
Sifa za Mpiga Kura
Ibara ya 5 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imempa haki kila raia aliyetimiza umri wa miaka kumi na minane kupiga kura.Kwa mujibu wa vifungu vya 13(1), 13 (2), 35C, 61 (3)(a) na 63(1) vya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 pamoja na kifungu cha 38 (1) cha Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Madiwani), Sura ya 292,Ili mtu aweze kupiga kura anatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:-
(i) Awe amejiandikisha katika Daftari la kudumu la wapiga kura:
(ii) Awe ana Kadi ya Mpiga Kura iliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi;
(iii) Awe katika kituo alichojiandikisha kupiga kura
Sheria ya Taifa ya uchaguzi inamruhusu mtu kupiga kura kwa kufuata utaratibu ufautao:
(i) Mpiga Kura anatakiwa kwenda kwenye kituo cha kupigia kura alichojiandikisha akiwa na kadi yake ya kupigia kura.
(ii) Mpiga kura anatakiwa kupanga mstari akiwa kituo cha kupigia kura na kusubiri hadi zamu yake ya kupiga kura itakapowadia.
(iii) Mpiga kura anatakiwa afuate maelekezo yote atakayopewa na msimamizi wa kituo muda wote akiwa kituoni.
(iv) Baada ya kumaliza kupiga kura, mpiga kura anatakiwa kurudi nyumbani.
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2024 Urambo . All rights reserved.