UTANGULIZI
Wilaya ya Urambo ni kati ya Wilaya Nane (8) zinazounda Mkoa wa Tabora. Wilaya hii ilianzishwa tarehe 19/07/1975 kwa namba za utambuzi GN of 185 of 1980 baada ya kugawanywa Halmashauri ya wilaya ya Tabora vijijini na Urambo; wilaya ya Urambo ina Tarafa mbili za Urambo na Usoke, Kata 18, Vijiji 59 na Vitongoji 254. Mwaka 2013, Halamshauri ya wilaya ya Urambo iligawanya pia katika Hamashauri mbili yaani Urambo na Kaliua.
Mipaka ya Halamshauri ya Wilaya ya Urambo
Wilaya hii imepakana na Wilaya ya Sikonge na Uyui kwa upande wa Mashariki, na inapakana na Wilaya ya Mpanda (Mkoa wa Katavi) kwa upande wa Kusini, kwa upande wa Kaskazini Magharibi inapakana na Wilaya ya Kaliua.
Ukubwa wa Eneo Halamshauri ya wilaya ya Urambo ina ukubwa wa eneo lenye kilometa za mraba Elfu sita miamoja kumi na moja ( km2 6,110) sawa na asilimia nane (8%) ya eneo la Mkoa wa Tabora. Makao makuu ya Wilaya yapo katika mji mdogo wa Urambo umbali wa kilometa takribani tisini (90 ) kutoka Tabora Mjini |
IDADI YA WATU
Kulingana na sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, Wilaya ya Urambo ina jumla ya wakazi wapato 192,781, (Nyamwezi ,Sukuma,Waha,Wafipa,Wasumbwa na wengineo) kati yao Wanaume 95,997 sawa na 49.80% na Wanawake 96,784 sawa na 50.2% . Wilaya ina jumla ya kaya 32,675 kwa wastani wa ukubwa wa kaya moja ni watu 5.9 ongezeko la watu kwa mwaka inakisiwa kuwa 4.8%.
VIONGOZI WETU
a) | b) |
HALI YA UCHUMI NA MAENDELEO YA WILAYA.
Uchumi wa Wilaya unategemea zaidi kilimo ambacho kinaajiri takribani asilimia 80 ya wakazi wote wa Wilaya hii. Mapato yanayotokana na ufugaji, Uvuvi, Ufugaji wa nyuki na shughuli za viwanda vidogo vidogo ni ajira mbadala zinazochangia katika pato la wakazi wetu.
Pato la Wilaya ya Urambo katika mwaka 2012/2013 hadi Desemba, 2012 lilikuwa Tshs. 77,822,778,064/= ikilinganishwa na idadi ya watu 192,781 na hivyo pato la mtu ni sawa na Tshs. 403,685/=. Aidha wastani wa pato la mtu kwa mwaka liliongezeka kutoka Tshs. 172,000/=mwaka 2002 hadi Tshs. 403,685/= mwaka 2012, sawa na ongezeko la Tshs. 231,685/=.
Hali ya Hewa
Hali ya hewa ya Halmashauri ya wilaya ya Urambo ni ya Kitropiko inatawaliwa na vipindi vikuu viwili kama ifuatavyo:-
|
Hali ya Joto ni kati ya 15˚C na 22˚C, joto uongezeka Mwezi wa Tisa, na hali ya |
HALI YA ULINZI NA USALAMA
Hali ya ulinzi na usalama katika Wilaya yetu kwa ujumla ni nzuri; na hii inachangiwa na uwepo wa ulinzi shirikishi kupitia Polisi jamii. Mpango huu muhimu ni wa kudumu kwa kushirikisha jeshi la mgambo katika suala la ulinzi kwa kuwatambua, kuwajali na kuwathamini.
Hata hivyo wilaya inaendelea kukabiliana na matukio mara kwa mara ya makosa ya jinai yakiwemo ya unyang’anyi wa kutumia silaha na nguvu, Uvunjaji, Wizi wa pikipiki,Wizi wa mifugo,kuchoma nyumba moto n.k. Mauaji yanayotokea katika Wilaya hii mara nyingi yanatokana na kulipiza kisasi, imani za kishirikina na matukio machache ya kugombea mali.
Kufuatia hali hiyo wilaya inashirikiana na Wilaya jirani katika mkakati wa kuimarisha Ulinzi na usalama na kubadilishana taarifa za kiuharifu miongoni mwetu na Wilaya zinazotuzunguka.
HALI YA UTOAJI HUDUMA KISEKTA
Shughuli ambazo zimekuwa zikitekelezwa na Wilaya kisekta katika utoaji wa huduma za kijamii na kiuchumi kama ifuatavyo:-
SEKTA YA UTAWALA NA UTUMISHI.
Wilaya ina jumla ya watumishi 1,458 kutoka katika kada mbalimbali za utumishi kama zifuatavyo:- Utawala na Utumishi 100, Elimu Sekondari 209,Elimu Msingi 835 , Afya 215, Kilimo Umwagiliaji na Ushirika 15,Mifugo na Uvuvi 9,Ardhi na Maliasili 6, Maji 7, Ujenzi 18, Watendaji wa Vijiji 43 na Usafi na Mazingira 1.
CHANGAMOTO
Watumishi walioajiriwa kuomba kuhama kufuata wenzi wao baada ya kukaa muda
Ufinyu wa bajeti
Utoro kazini
Watumishi wapya Kushindwa kuripoti na Serikali kutoleta watumishi kulingana na ikama iliyoidhinishwa.
gana na ikama iliyoidhinishwa.
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.