Kitengo cha Tehama
Kitengo cha TEHAMA, na Mahusiano
Kitengo cha (TEHAMA) kimeanzishwa mwaka 2010 kwa kuunganisha kitengo cha Teknolojia ya Habari Mawasiliano na Mahusiano . Kitengo hiki kinaongozwa na Sera ya TEHAMA (2003), na Sera ya Utangazaji Habari (2004). Ibara ya 18 yakatiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Idadi ya Watumishi:
Kwa sasa kitengo cha TEHAMA kina watumishi watatu, mmoja mwenye ajira ya kudumu na wawili ni ajili ya muda.
HUDUMA KWA JAMII:
Kitengo cha TEHAMA kinasimamia mifumo mbalimbali inayotoa huduma kwa jamii ikiwemo
1. Mfumo wa Kielektroniki wa matibatu (GoT-HoMIS v3)
2. Mfumo wa Kielekroniki wa Uhasibu wa utoaji wa Taarifa katika vituo vya kutolea huduma (FFARS, mfumo huu unatumiwa na idara za Elimu Msingi, Sekondari na Afya
Kama unahitaji msaada wa kitaalamu kutoka kitengo cha TEHAMA wasiliana na Mkurugenzi Mtendaji(W) URAMBO (0784828287) kisha atakuunganisha na mtaalamu mmojawapo wa TEHAMA.
Kitengo hiki kinasimamia na kuratibu matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, na kutoa usaidizi wa kiufundi kwa mfumo jumuishi wa Kompyuta na mifumo mingine pamoja na Vifaa vya TEHAMA.Aidha, Kitengo kinatoa huduma za kitaalamu kuhusiana na matumizi ya TEHAMA kama ifuatavyo;
a) Kushughulikia utekelezaji wa Sera ya Serikali Mtandao, miongozo, kanuni na viowango vya matumizi na utekelezaji wa TEHAMA.
b) Kuweka mifumo na mitandao ya Serikali Mtandao.
c) Kutoa msaada wa matumizi sahihi ya teknolojia ya Habari na Mawasiliano.
d) Kuhakikisha vifaa vya TEHAMA vinahudumiwa kiufundi na kwa wakati..
e) Kutoa msaada wa kiufundi na utaalamu wa kununua Vifaa na Mifumo ya TEHAMA .
f) Kuhudumia na Kuhuisha mifumo na miundombinu ya mawasiliano (LAN/WAN).
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.