Mbunge wa Jimbo la Urambo Mhe. Margareth Sitta alikabidhi Gari jipya la kubebea wagonjwa (Ambulance) katika kituo cha Afya Ussoke mnamo tarehe 15.02.2025 ikiwa ni katika jitihada za kuhakikisha huduma bora za Afya zinapatikana kwa ufanisi zaidi na kuwafikia wananchi kama ambavyo Serikali ya Awamu ya Sita imekusudia.
Mhe. Margaret Sitta alikabidhi gari hilo katika kituo cha Afya Ussoke akiwa katika Ziara ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilayani Urambo. Ziara hii iliyoongozwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilayani Urambo Ndg. Mussa Shabani na kuhusisha Wajumbe wa Halmashauri hiyo ya CCM, Mkuu wa Wilaya ya Urambo Mhe. Dkt. Khamis Mkanachi, Mhe. Mbunge wa Jimbo Margareth Sita,Timu ya Wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Urambo iliyoongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Bi. Grace Quintine pamoja na Wakuu wa Taasisi mbalimbali ikiwemo RUWASA, TANESCO pamoja na TARURA na Wataalamu wao. Ziara hii ilikuwa maalumu kwa ajili ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Miradi mbalimbali ya kimkakati inayolenga kutatua changamoto mbalimbali kwa wakazi wa Urambo.
Sambamba na hilo Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Urambo ilitembelea miradi mingine ya kimkakatii inayotekelezwa wilayani hapa ukiwemo Mradi Mkubwa wa maji ya Ziwa Victoria, mradi unaotarajiwa kumaliza tatizo la maji Wilayani Urambo na Wilaya nyinginezo kama Kaliua na Sikonge pamoja na Mradi wa Ujenzi wa Bwawa la Maji katika Kijiji cha Kalemela "A" mradi wenye thamani ya Bilioni 5.9.
Aidha Mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kutoka Tabora kuelekea Kigoma Pamoja na kituo kikubwa cha Kupokea na Kupoza umeme ambacho kinatarajia kuanza kutumika hivi karibuni vilitembelewa.
Ikumbukwe kuwa Wilaya ya Urambo imepokea fedha nyingi zilizoletwa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Juhudi za Mbunge wa Jimbo la Urambo Mhe. Margaret Sitta za kuhakikisha Urambo inapata huduma Bora za kijamii ikiwemo huduma za Afya, Maji, Umeme pamoja na Elimu.
Kazi iendelee
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.