Katika Mkutano wa Baraza la Madiwani la kupokea taarifa za utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Kamati za Halmashauri, Mhe. Dkt. Khamis Mkanachi alieleza wazi kuwa, katika kuhakikisha mapato ya Halmashauri yanakusanywa kikamilifu, Cheo hakitomsaidia mtu yeyote kujinasua katika kesi ya Utoroshaji ama Ulanguzi wa Tumbaku.
Mhe. Dkt. Mkanachi amewaasa Wahe. Madiwani na wageni waalikwa katika kikao hicho kuwa, kama mtu anahitaji kunufaika na tumbaku basi alime tumbaku, na yule anayetaka kununua tumbaku na akawe kampuni ya ununuzi wa tumbaku. Hatua hii imekuja katika muendelezo wa Serikali kuhakikisha mkulima ananufaika na zao la tumbaku na kuinuka kiuchumi.
Ikumbukwe kuwa Wilaya ya Urambo ni moja kati ya Wilaya Kinara katika uzalishaji wa Tumbaku katika Mkoa wa Tabora na Nchini Tanzania, Hivyo mapato ya Halmashauri ya Wilaya ya Urambo yanategemea zaidi Tumbaku. Pamoja na Mapato ya Halmashauri Zao la Tumbaku ni Msingi pia wa uchumi kwa Wananchi wa Wilaya Hii, Hivyo basi ni jambo la Msingi kupambania zao la Tumbaku.
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.