Urambo,
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Bi. Grace Quintine tarehe 29.09.2025 akiwa pamoja na wajumbe wa timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Urambo (CMT), amewapokea Madaktari Bingwa 6 wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambao wameweka kambi ya siku tano kwa ajili ya kutoa huduma za Kibingwa kwa Wananchi wa Wilaya ya Urambo.
Madaktari hawa Sita Walioambatana na Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya Dkt. Bundala wanatarajia kutoa matibabu ya kibingwa ya
1. Magonjwa ya upasuaji
2. Magonjwa ya ndani kama vile shinikizo la juu la damu au kisukari
3. Magonjwa ya wanawake na ukunga
4. Magonjwa ya kinywa na meno
5. Magonjwa ya watoto na watoto wachanga
Aidha Bi. Grace Quintine amemshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuwaleta madaktari hawa kila mwaka ili watoe huduma kwa wananchi, na kuwapunguzia adha ya kufuata huduma hizi katika hospitali kubwa Nchini.
Bi. Grace Quintine aliendelea kwa kusema kuwa, kutokana na juhudi kubwa za Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha Hospitali ya Wilaya ya Urambo, madaktari hawa watakwenda kufanya kazi zao katika mazingira bora kutokana na uwepo wa majengo mapya pamoja na vifaa tiba vya kisasa vya kutosha.
Naye Mganga Mkuu wa Wilaya ya Urambo Dkt. David Manyama ameeleza kuwa, Madaktari hawa watakuwepo na kutoa huduma za afya katika Hospitali ya Wilaya kuanzia tarehe 29.09.2025 hadi tarehe 03.10.2025 kwa gharama nafuu sana.
Aidha Dkt. Manyama amesema kuwa ujio wa madaktari bingwa hawa unakwenda kusaidia kutibu wagonjwa wengi waliokuwa na changamoto mbalimbali na kushindwa kufuata huduma hizo katika hospitali kubwa, na pia kuwaongezea ujuzi wataalamu wa afya katika hospitali ya Wilaya ya Urambo.
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.