Urambo, Tabora
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Mkoani Tabora, Bi. Grace Quintine ametembelea miradi anuai inayotekelezwa katika Kata mbalimbali za Tarafa ya Urambo na Ussoke Wilayani Urambo yenye thamani ya Tsh 3,507,536,700 inayotekelezwa katika Wilaya ya Urambo kupitia Fedha kutoka Serikali kuu na Mapato ya Ndani ya Halmashauri.
Bi. Quintine amefanya ziara hiyo siku ya Jumanne Septemba 30, 2025 na Jumatano 01.10.2025 katika maeneo ambayo miradi inatekelezwa na kuwataka mafundi wanaojenga miundombinu hiyo kuzingatia thamani ya fedha kwa lengo la kuhakikisha inadumu na kutoa huduma kwa muda Mrefu.
Aidha, amewataka wataalamu wa Halmashauri ambao wanahusika na kusimamia miradi hiyo kuwa karibu na miradi hiyo kwa lengo la kuhakikisha inakamilika kwa wakati na kwa ubora wa hali ya juu vinginevyo watawajibika wao wenyewe kushughulika na mapungufu yatakayojitokeza.
Sambamba na hilo Bi. Grace Quintine aliyeambatana na timu ya Wataalamu, ametembelea miradi inayofadhiliwa na Wadau wa Maendeleo ambao ni SEQUIP, BOOST na GPE-TSP yenye thamani ya Tsh. Bilioni 2,190,281,126, miradi inayojengwa kwa fedha kutoka serikali Kuu yenye Thamani ya fedha Bilioni 1,256,135,134 na Mapato ya Ndani yenye thamani ya Milioni 61,120,440.
Miradi yote iliyotembelewa inatekelezwa katika sekta mbalimbali ikiwemo Sekta ya Afya kupitia ujenzi wa vituo vya Afya, zahanati n.k, Idara ya Elimu ambapo serikali inajenga Vyumba vya Madarasa, Mabweni na Matundu ya Vyoo Pamoja na Mifugo kupitia ujenzi wa majosho.
Hata hivyo Bi. Quintine amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuona umuhimu wa Kutoa fedha nyingi za Miradi kwa ajili ya Wanaurambo, hivyo ni wajibu wa kila anayehusika kukamilisha dhamira ya Serikali ya awamu ya Sita ya kuwahudumia Wananchi kwa Vitendo.
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.