Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri yuko katika ziara ya kikazi kuhamasisha kilimo bora cha Pamba kwa musimu wa mwaka huu, akiwa Wilayani Urambo Machi 15 hadi 16, 2018 amewataka wakazi wa Wilaya ya Urambo kuwa makini kwa kutoa taarifa sahihi wakati wa zoezi la uandikishaji kwa ajili ya vitambulisho vya Taifa ili watu wasiostahili wasije wakajipenyeza na kupatiwa vitambulisho bila kustahili.
Akizungumza katika Kijiji cha Ussoke Mlimani alisema kuwa wananchi wanatakiwa kufichua watu wote wasio raia ambao wanataka kujiandikisha ili waweze kupata vitambulisho kinyume cha sheria.
“Ili zoezi hili liwe na tija kwao na Taifa ni vema wananchi mkatoa ushirikiano kwa watendaji wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa yaani NIDA, na kwa viongozi wa Wilaya pale wanapomtilia shaka mtu anayetaka kujiandikisha ili uchunguzi ufanyike kuzuia udanganyifu huo” alisema hayo Mkuu wa Mkoa.
Aidha aliwakumbusha wananchi ya kuwa huko nyuma Urambo ilikuwa sehemu ya makazi ya Wakimbikizi kutoka nchi jirani hasa sehemu za Ulyankulu na walikuwepo baadhi yao walio jipenyeza na kuweka makazi bila kufuata utaratibu.
Alisema ni jukumu la kila mkazi wa Urambo ambaye ni mzalendo kufichua mbinu chafu kama zinataka kufanyika ili kuficha ukweli wa mtu kwa makusudio ya kutaka kumpa kitambulisho mgeni.
Pia Mkuu wa Mkoa alitoa wito kwa Wakazi wote wa Mkoa huo ambao wana sifa kuendelea kujitokeza kwa wingi kwenda katika maeneo yalipopangwa ili kujiandikisha kabla ya muda wa mwisho wa zoezi hilo.
Alisema kitendo cha baadhi ya watu kupenda kujiandikisha siku za mwisho kimekuwa kikisababisha msongamano na usumbufu kwa wananchi na kuongeza ili kuepuka ili waende mapema vituoni.
Imeandaliwa na
Kitengo cha TEHAMA(W) kwa kushirkiana na Afisa Habari(Mkoa)
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.