Mnamo tarehe 20.02.205 Kampuni ya Japan Tobacco International (JTI) ilikabidhi hundi ya mfano yenye thamani ya Tsh. 235,622,500/= kwa lengo la kuendeleza uboreshaji wa miundombinu mbalimbali ikiwemo uzio katika shule ya Wasichana ya Margaret Sitta.
Hundi hiyo imekabidhiwa katika hafla fupi iliyohusisha usomaji wa taarifa ya maendeleo ya shule hiyo tangu kuanzishwa kwake. Aidha kupitia taarifa hiyo, imebainika kuwa Shule hiyo imeleta mapinduzi makubwa katika sekta ya Elimu Wilayani Urambo, kwani imekuwa ikiongoza na kushika nafasi nzuri katika Mitihani ya Kitaifa. Ikumbukwe kuwa Shule hii ilijengwa na Kampuni ya JTI kupitia mpango wa kurudisha kwa Jamii ambapo zaidi ya Miliooni 900 ilitumika.
Aidha, Halfla hiyo ilihudhuriwa na Wageni mbalimbali akiwemo Mhe. Anne Makinda, Mhe. Dkt. Khamis Mkanachi - Mkuu wa Wilaya ya Urambo, Mhe. Margaret Sitta - Mbunge wa Jimbo la Urambo, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Urambo Ndg. Shabani Mussa, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Mhe. Adam Malunkwi, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Bi. Grace Quintine pamoja na Wataalamu mbalimbali kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Urambo.
Aidha ulikuwepo Uongozi wa kampuni ya JTI ambao ndiyo chachu ya mafanikio ya shule hiyo, ambapo umeonyesha kufurahishwa na ufaulu wa wanafunzi katika shule hiyo na kuahidi kuwa yote yaliyoombwa watayashughulikia kadiri itakavyowezekana kutokana na mafanikio yaliyofikiwa na shule hiyo.
Sambamba na hilo imeelezwa kuwa Kampuni ya JTI imekuwa kampuni Bora na ya Mfano kwa Makampuni mengi ya Tumbaku, ambapo hulipa wakulipa kwa Wakati na kuwasaidia Wakulima ili waweze kupata mavuno yaliyo bora. Hivyo kwa Kutambua mchango wa JTI kwa kujenga shule hiyo, Halmashauri ya Wilaya ya Urambon iliweza kuongeza Madarasa Matatu katika shule hiyo ya Kitaifa ya Wasichana.
Kazi iendelee
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.