Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Urambo ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Adam Malunkwi, imefanya ziara ya kutembelea Miradi mbalimbali katika robo ya tatu ya mwaka 2024/2025, ikiwemo mradi wa umaliziajj wa Kituo cha Afya katika Kata ya Ukondamoyo ambacho kinatarajia kunufaisha wananchi wa Kata ya Ukondamoyo na kupunguza umbali wa zaidi ya Km 16 kufuata huduma katika Hospitali ya Wilaya ya Urambo pale inapobidi kupata huduma katika hospitali ya Wilaya.
Kituo cha Afya katika Kata ya Ukondamoyo kipo katika hatua ya umaliziaji pia ni mradi ambao umelenga kuimarisha utoaji wa huduma za afya katika Wilaya ya Urambo kwa kusogeza huduma karibu na wananchi na kuwapunguzia umbali wa kufuata huduma hiyo katika hospitali ya Wilaya.
Katika ziara hiyo iliyofanyika leo tarehe 24.04.2025, Kamati hiyo pamoja na maelekezo mengine, iliweza kuwaagiza wasimamizi wa mradi huo kuongeza kasi katika umaliziaji ili Kituo hicho kianze kuwahudumia wananchi wa kata hiyo hivi karibuni.
Aidha Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango iliweza kutembelea mradi wa ujenzi wa nyumba mbili za Wakuu wa Idaza za Halmashauri ya Wilaya ya Urambo, na kupongeza hatua iliyofikiwa na namna ambavyo mradi huo unatekelezwa.
Nyumba hizo zitakapokamilika zitasaidia katika kuwasogeza watumishi (wakuu wa idara) karibu na mahala pa kazi ili kuongeza ufanisi na ari ya kutoa huduma kwa Wananchi wa Urambo.
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.