Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Tabora imefanya Ziara katika Wilaya ya Urambo kwa ajili ya kukagua Miradi itakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru mwaka 2024. Kamati hiyo iliyoongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora Ndg. Dkt. John Rogath Mboya Pamoja na Timu ya wataalamu mbalimbali imekagua Miradi hiyo itakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru mwaka 2024.
Aidha, Kamati hiyo iliambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama kutoka Wilayani Urambo inayoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Urambo Dkt. Khamis Athumani Mkanachi pamoja na wataalamu kutoka Taasisi mbalimbali ikiwemo RUWASA na TARURA. Aidha Ziara hiyo ilijumuishaTimu ya wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Urambo ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Bi. Grace Quintine.
Mkuu wa Wilaya ya Urambo Mhe. Dkt. Khamis Athumani Mkanachi ameieleza Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Tabora kuwa Wilaya ya Urambo inatarajia Kuukimbiza Mwenge wa Uhuru kwa Umbali wa Kilomita 98 na Kupitia Miradi yenye thamani ya Jumla ya Tsh Bilioni 8.297. Pamoja na Hilo Dkt. Mkanachi amesisitiza kuwa Urambo itaendelea kuongoza Kitaifa kama ambavyo ilifanya mwaka jana (2023) kwani Urambo imejiandaa vyema kuupokea na kuukimbiza Mwenge wa Uhuru.
Miradi inayotarajia kupitiwa na Mwenge wa Uhuru mwaka 2024 inajumuisha Shamba la miti la Imalamakoye lenye thamani ya Tsh. 58,563,500.00, Shule ya Sekondari Igunguli yenye thamani ya Tsh 603,890,562.00 fedha kutoka Mradi wa SEQUIP, mradi wa Bwawa la Maji katika Kijiji cha Kalemela "A" wenye thamani ya Bilioni 5.9 fedha kutoka Serikali Kuu, Ujenzi wa Vibanda 20 vya Biashara Katika Stendi ya mabasi vyenye thamani ya Tsh 110,000,000.00 fedha kutoka Mapato ya ndani, Majengo Manne katika Hospitali ya Wilaya ya Urambo yenye thamani ya Tsh 900,000,000.00 fedha kutoka Serikali Kuu, Mradi wa Ujenzi wa Barabara kwa kiwango cha lami wenye thamani ya Tsh 712,000,000.00 Fedha kutoka Serikali Kuu, Mradi wa Kikundi cha Vijana waendesha pikipiki za abiria (Bodaboda) cha UMOJA MATANKI MANNE Mradi wenye thamani ya Tsh 13,000,000.00 fedha kutoka Mapato ya ndani. Aidha katika Miradi hiyo Miradi Minne (4) itawekewa Jiwe la Msingi, Miradi Miwili (2) Itazinduliwa na Miradi Miwili itatembelewa ili kutazama Shughuli zinazoendelea katika Miradi Hiyo.
Pamoja na kukagua Miradi hiyo Kamati hiyo ilipata wasaa wa kukagua eneo la mapokezi na Mkesha wa Mwenge wa Uhuru na Kamati hiyo ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Tabora ilitoa maoni yake kuhusu Utayari wa Miradi hiyo katika Kuelekea mapokezi na Mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoani Tabora na Wilayani Urambo.
Aidha Wananchi wa Urambo wanasisitizwa kushiriki kikamilifu katika Maandalizi ya kuupokea na kuukimbiza Mwenge wa Uhuru Wilayani Urambo, kwani Mwenge wa Uhuru ni Mali ya Watanzania wote. Ziara hii ni muendelezo wa maandalizi ya Kuupokea Mwenge wa Uhuru Mkoani Tabora Mwezi Agosti, 2024.
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2024 Urambo . All rights reserved.