Kamati ya Ushauri Wilaya ya Urambo (DCC) imepitia, imejadili na kupitisha Rasimu ya Bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Urambo kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026 kwa kauli moja.
Rasimu hiyo imepitishwa na DCC tarehe 29.01.2025 wakati wa kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo na kuhudhiriwa na makundi mbalimbali, wakiwemo viongozinwa Vyama vya Siasa, Viongozi wa dini n.k
Kikao hicho kimeongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Dkt. Khamis Mkanachi Mkuu wa Wilaya ya Urambo aliyeongozana na Katibu Tawala Ndg. Innocent Nsena.
Wajumbe wa Kamati walishauri mambo mbalimbali ikiwemo utoaji wa Mafunzo ya mfumo wa Manunuzi ili kutekeleza Bajeti kwa ukamilifu na kwa wakati kwani changamoto kubwa hutokana na mfumo huo kutofahamika na wengi.
Pia DC Mkanachi amesema Miradi iliyopangwa kukamilishwa hasa zahanati mbili ambazo ni zahanati ya Mwinyi na Ukwanga ikamilishwe kwa wakati ili Wananchi waanze kupata huduma kwa ukaribu na kwa Wakati.
Aidha, Wajumbe wa DCC Wamepongeza maandalizi yaliyofanywa na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji na Wataalamu wake kwa Rasimu hiyo.
Kazi iendelee
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.