Urambo, Tabora
Timu ya Madaktari wa utengamano kutoka hospitali ya Kitete imeweka katika hospitali ya wilaya ya Urambo ili kutoa huduma kwa watoto wenye changamoto ya utindio wa ubongo na ukuaji.
Akiwapotea wataalamu hao, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Urambo Dkt. David Manyama amesema kuwa, Hospitali ya wilaya ya Urambo imekuwa ikiwapokea wagonjwa wa utengamano hivyo ujio wa wataalamu hao umekuwa msaada mkubwa sana kupitia matibabu yatakayotolewa pamoja na kuwaongezea uzoefu wataalamu wa hospitali ya Wilaya ya Urambo.
"Tumekuwa tukipata wagonjwa wengi wa aina hiyo, hivyo imekuwa wakati mzuri sana kuwapata wataalamu hawa kutoka Hospitali ya Kitete kwa sababu watasaidia kutoa huduma kwa wagonjwa wetu"
Pia ameupongeza uongozi wa hospitali ya Kitete kwa kuwaruhusu wataalamu hao ili kutoa huduma katika wilaya nyingine ili kuhakikisha huduma bora za afya zinawafikia wananchi wote kama inavyoelekezwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa upande wake Dkt. Leonard Makey ambaye ni mtaalamu wa utengamano kutoka Hospitali ya Kitete amesema kuwa, watatoa huduma kwa wilaya ya Urambo kwa muda wa siku mbili kuanzia tarehe 24 - 25 Septemba 2025. Ameongeza kwa kusema, Wilaya ya Urambo ina idadi kubwa ya watoto wenye changamoto ya utindio wa ubongo na ukuaji ndiyo maana wameweka kambi katika hospitali hiyo.
Kazi iendelee
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.