Katika kuendana na mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia pamoja na utunzaji wa mazingira, Halmashauri ya Wilaya ya Urambo imekabidhi vishikwambi 24 kwa Waheshimiwa Madiwani ili vitumike katika vikao na shughuli nyingine za Halmashauri.
Zoezi la ugawaji wa Vshikwambi hivyo limeshuhudiwa na Katibu Tawala Wilaya ya Urambo Ndg. Innocent Nsena, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Masudi I. Masudi pamoja na wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo.
Vishikwambi hivyo vimetolewa katika Kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika tarehe 31.01.2025 katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo.
Aidha, Kupatikana kwa vishikwambi hivi kutasaidia katika kuboresha na kupunguza gharama pamoja na muda mrefu wa kuzalisha Makabrasha kwa ajili ya vikao mbalimbali vya kisheria.
Aidha Wahe. Madiwani wa Kata za Urambo wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Mhe. Adam Malunkwi wameonyesha furaha baada ya kupokea vishikwambi hivyo ambavyo vitakuwa mbadala wa matumizi ya Makabrasha.
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.