Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo, Mnamo tarehe 16.02.2025 walifanya Ziara ya kutembelea Eneo la hifadhi ya Jamii Uyumbu (WMA) iliyoandaliwa na ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji kwa ajili ya kuona shughuli zinazofanyika katika WMA hiyo.
Ziara hii ilimhusisha Mkuu wa Wilaya ya Urambo Mhe. Dkt. Khamis Mkanachi, Katibu Tawala Ndg. Innocent Nsena, Mbunge wa Jimbo la Urambo Mhe. Margareth Sitta, Waheshimiwa Madiwani wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Adam Malunkwi pamoja na Wakuu wa Divisheni na Vitengo vya Halmashauri wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Bi. Grace Quintine.
Aidha Ziara hii ni muendelezo wa Ziara ya Mafunzo iliyofanyika Mwaka 2024 Wilayani Serengeti kwa ajili ya kujifunza uendeshaji wa Maeneo ya Hifadhi za jamii ili kukuza pato la Halmashauri.
Aidha Ugeni huu uliweza kupokelewa na kuzungumza na Mwekezaji pamoja na uongozi wa WMA na kujadili changamoto na masuala mbalimbali kwa ajili ya kuinua WMA ya UYUMBU.
Kazi iendelee
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.