Urambo - Tabora
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Bi. Grace Quintine amesisitiza Usikivu na uelewa katika mafunzo ya utawala bora kwa Wenyeviti wa vijiji Wilayani Urambo, ili kujifunza na kuelewa namna ya kuongoza pamoja na mipaka ya majukumu ya Wenyeviti wa vijiji.
Bi. Grace Quintine ameyasisitiza hayo wakati akifungua mafunzo kwa Wenyeviti wa vijiji tarehe 26. 06.2025 katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo yenye Lengo la Kuboresha Utendaji.
Aidha Bi. Quintine ameeleza kuwa dhumuni la mafunzo hayo ji kusaidia kueleza mipaka ya kimajukumu pamoja na kuepusha migogoro baina ya Wenyeviti pamoja na Watendaji wao.
Aidha Bi. Grace Quintine ameendelea kwa kusema kuwa, Mafunzo hayo ni Mpango wa Serikali wa kuhakikisha Wenyeviti wa vijiji wanajengewa uwezo wa utekelezaji wa majukumu, hivyo ndiyo maana Wawezeshaji wamewasili kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa (Hombolo) ili waweze kuelekeza vyema.
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.