Urambo, Tabora.
"Ahsante Mhe. Margaret Sitta, ni Wabunge wachache sana Wanaojali na kuwasikiliza Watumishi wa Umma"
Hayo yamezungumzwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Bi. Grace Quintine katika kikao maalumu cha Mbunge wa jimbo la Urambo Mhe. Margaret Sitta pamoja na Watumishi wa Makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Urambo. Kikao hicho kimefanyika leo tarehe 28.02.2025 katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo, ambapo ni kikao maalumu kwa ajili ya kusikiliza changamoto zinazowakumba watumishi wa Umma katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Aidha Bi. Grace Quintine amempongeza Mbunge wa Jimbo la Urambo kwa juhudi zake za dhati za kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo Maji, Umeme na Elimu, changamoto ambazo zinawagusa Watumishi wa Umma moja kwa moja kama Wananchi wa Urambo. Pamoja na pongezi hizo Mkurugenzi Quintine alisema kuwa anaamini changamoto mbalimbali zilizosikilizwa na Mhe. Mbunge zitakwenda kutatuliwa kutokana na uzoefu wake na nia ya dhati ya kuzitatua.
Sambamba na hilo Mhe. Margareth Sitta alieleza kuwa ataendelea kuzipokea na kuzishughulikia changamoto hizo kadiri itakavyowezekana.
Aidha Mhe. Mbunge ameendelea kufanya vikao na watumishi ambapo aliweza kufanya kikao pamoja na watoa huduma za afya katika Hospitali ya Wilaya ya Urambo ambao kwa pamoja wameungana na Watumishi wa Makao makuu kwa kutoa shukrani kwa vikao hivyo ambavyo ni nadra sana kufanywa na Waheshimiwa Wabunge.
Kwa upande wake Mhe. Mbunge wa Jimbo la Urambo Mhe. Margaret Simwanza Sitta amempongeza Mkurugenzi Mtendaji Bi. Grace Quintine kwa ufuatiliji wake wa karibu wa fedha za Miradi zinazoletwa kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Urambo kwa lengo la kuboresha huduma kwa Watanzania wa Urambo.
Kazi iendelee
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.