Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Tabora Mhe. Jaqueline Andrew siku ya tarehe 03.03.2025 ametoa msaada wa mahitaji mbalimbali kama Mashuka, Neti, Beseni, Sabuni n.k kwa ajili ya kusaidia wanawake mbalimbali waliojifungua.
Mhe. Jaqueline ametoa vitu hivyo ikiwa ni kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake ambapo kwa Wilaya ya Urambo mambo mbalimbali yalifanyika ikiwemo kufanya Usafi katika Hospitali ya Wilaya ya Urambo pamoja na kuchangia damu.
Siku ya Kimataifa ya Wananawake inatarajiwa kuadhimishwa tarehe 8 Machi, 2025 ambapo kwa Mkoa wa Tabora sherehe hizo zitafanyika Wilayani Nzega na Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Paul Chacha.
Aidha kwa Wilaya ya Urambo Sherehe hizi zinafanyika Leo tarehe 04.03.2025 na Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Urambo Mhe. Dkt. Khamis Mkanachi. Sherehe hizi zitaanza kwa Matembezi kuelekea katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo ambapo litafanyika Kongamano.
Siku hii ni Muhimu sana kwa ajili ya kutambua mchango wa Wanawake katika Jamii ambapo hufanyika kila mwaka tarehe 08 Machi.
"Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji"
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.