Urambo - Tabora
Katika kuhakikisha malengo ya Serikali katika Matumizi ya teknolojia katika utendaji kazi, Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo wamepokea mafunzo muhimu ya Mfumo wa kielektroniki wa utendaji (Pepmis) kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Mafunzo haya yalifanyika tarehe 24.06.2025 katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo, na kuwasilishwa na Bi. Cecilia Meela, na kuhudhuriwa na Katibu Tawala Wilaya ya Urambo Ndg. Innocent Nsena, Mkurugenzi Mtendaji Bi. Grace Quintine pamoja na Maafisa wengine wa Halmashauri.
Aidha Lengo la Mafunzo haya ni kuongeza ufanisi na kutekeleza mkakati wa Serikali wa kuhakikisha Watumishi wanatekeleza majukumu yao na kufanyiwa tathmini kupitia mfumo wa Kielektroniki (Pepmis).
Mafunzo hayo ya ufanyaji wa tathmini yamekuja wakati sahihi kwani ni mwishonwa mwaka wa fedha 2024/2025 ambapo watumishi hufanyiwa tathmini ya utendaji wao kwa mwaka mzima.
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.