Mkuu wa Wilaya ya Urambo Mhe. Dkt. Khamis Mkanachi amezindua Zahanati ya Kinhwa iliyopo kata ya KIloleni Wilayani Urambo na kuwapongeza Viongozi wa Kata na Wananchi wa Kata hiyo kwa ushirikiano wao katika Shughuli za Serikali.
Mhe. Dkt. Mkanachi alizindua Zahanati hiyo tarehe 25.04.2025 akiongozana na Katibu Tawala wa Wilaya, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya, Wataalamu kutoka Hospitali ya Wilaya ya Urambo katika Uzinduzi huo.
Wakati wa hotuba yake Mhe. Dkt. Mkanachi amesema ujenzi wa Zahanati hiyo ni Lengo la Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan la kusogeza huduma za afya karibu na Wananchi.
Mhe. Dkt. Mkanachi aliagiza Jeshi la Sungusungu kuhakikisha linaweka ulinzi wa hali ya juu kulinda Zahanati hiyo ambayo imewekewa vifaa tiba bora kwa ajili ya Wananchi wa Kinhwa na maeneo ya jirani.
Sambamba na hilo Diwani wa Kata ya Kiloleni Mhe. Salum Mtalu amemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kusimamia vizuri maendeleo ya Wilaya ikiwemo kukamilika kwa Zahanati ya Kinhwa inayoenda kusaidia katika utoaji wa hudumua bora sa afya kwa wananchi. Aliendelea kwa kumwombea kwa Mungu ili aweze kufanikisha jitihada za kuleta maendeleo katika Wilaya ya Urambo.
Kwa upande wa Wananchi wa Kata hiyo wametoa Pongezi kwa Serikali ya awamu ya Sita kwa kuwajengea zahanati hiyo kwani mwanzo walikuwa wakifuata matibabu kwenye makao makuu ya Kata, hivyo kuzinduliwa kwa Zahanati hiyo kutarahisisha upatikanaji wa huduma za afya katika eneo hilo.
Aidha Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Dkt. Gloria Dionis amesema faida ya Zahanati hiyo ni kutoa huduma ili kupunguza vifo vya wanawake wajawazito na Watoto, kuhudumia wazee wasioweza kwenda umbali mrefu pamoja na kutoa huduma kwa wananchi wa eneo hilo.
Ikumbukwe kuwa Zahanati ya Kinhwa hadi kukamilika kwake Fedha kiasi cha Tsh. Milioni Themanini na Tano imetumika, fedha hii ni kutoka Serikali kuu.
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.