Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Bi. Grace Quintine ametembelea zahanati ya Gereza la Kilimo Urambo inayotoa huduma kwa Askari Magereza, Watumishi, Wafungwa pamoja na Wananchi wa vijiji na maeneo yanayozunguka Gereza hilo.
Bi. Grace Quintine amefanya ziara hiyo tarehe 18.09.2025, akiambatana na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Urambo Dkt. David Manyama Nyambaya kwa ajili ya kukagua huduma zinazotolewa katika zahanati hiyo ili kujionea hali na Shughuli za Kitabibu zinazotolewa katika zahanati hiyo ya Gereza la Kilimo Urambo pamoja na Hali ya mazingira ya gereza la Nsenda.
Aidha Bi.Grace baada ya kukagua ameridhishwa na huduma zinazotolewa na kusisitiza kuendelea kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za afya katika zahanati hiyo. Aidha zahanati hiyo hutoa huduma mbalimbali za awali na zile ambazo hutolewa katika ngazi ya Chini ikiwemo huduma ya wajawazito na watoto wachanga kabla ya kufikishwa katika Vituo vya Afya na Hospitali ya Wilaya pale rufaa itakapohijitajika.
Pia ameahidi kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo itaendelea kushirikiana kwa karibu na Gereza la kilimo na itaendelea kutoa kipaumbele katika Sekta ya afya kama ambavyo Serikali inavyoelekeza ili kuhakikisha huduma bora zinapatikana kwa Wananchi wote Urambo.
Aidha Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt. David Manyama Nyambaya ameahidi kuhakikisha na kuendelea kutoa ushirikiano Mkubwa katika usimamizi shirikishi wa kusimamia huduma za Afya kati ya Magereza ya Nsenda na Halmashauri ya Wilaya.
Kwa upande wake Mkuu Gereza la Kilimo Urambo Joseph . W. Mzulama amemshukuruu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Bi Grace Quintine kwa ushirikiano mkubwa anaoutoa kwa Gereza la Kilimo pamoja na kuitembelea zahanati hiyo, ili kuhakikisha huduma bora za afya zinapatikana kwa Askari Magereza, Watumishi, Wafungwa pamoja na wananchi wa maeneo ya jirani.
Kazi iendelee
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.