Kamishina Mhe. Elibariki Bajuta Mkuu wa wilaya Urambo akiambatana na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji(W) Urambo na baadhi ya Wataalamu Jumatatu ya Novemba 6, 2023 wametembelea wahanga wa maafa ya mvua iliyoambatana na upepo mkali tarehe 05/11/2023 katika kijiji cha Uyogo Tarafa ya Urambo.
Akisoma taarifa kwa niaba ya Serikali ya Kijiji Bi. Rehema Shaban Mtendaji wa kijiji cha Uyogo amesema jumla ya paa za nyumba 12 zimeezuliwa na upepo pamoja na paa moja la jengo la zahanati ya kijiji cha Uyogo, amesema wananchi wamepoteza chakula na sehemu ya malazi lakini hakuna kifo kilichotokana na hathari hiyo.
Mhe. Bajuta ametoa pole kwa wananchi wote waliokumbana na kadhia hiyo na kumwagiza Mkurugenzi Mtendaji(W) kupitia Kamati ya Maafa Wilaya kufanya tathimini ya haraka kuhakikisha wananchi hao wanapata msaada wa kibinadamu ili waweze kuendelea na shughuli zao za kila siku.
Mhe. Bajuta amewaomba na kuwasihi wananchi wa Urambo kuzingatia tahadhali zote zinazotolewa na mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), na kila mmoja kufuatilia utabiri wa hali ya hewa unaotolewa na vyombo vya habari kisha kuchukua tahadhali kwa kipindi hiki cha mvua zilizoanza kunyesha wiki moja sasa hasa kwa watoto, mifugo na kuhakikisha hakuna uchafu kwenye mitaro ya maji iliyopo karibu na makazi yao.
Aidha, katika kata ya Ukondamoyo imeripotiwa mvua hiyo kusababisha kifo cha mtu mmoja mkazi wa kijiji cha Ifuta kitongoji cha Ibana Bi. Bernadeta Agustino Mihambo (33) aliyefariki kwa kupigwa na radi wakati akiwa ndani ya nyumba yake.
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2024 Urambo . All rights reserved.