Mhe. Magret Simwanza Sitta(MB) Jimbo la Urambo ndani ya Kambi ya Umitashumita 2022
Hamasa imeongezeka kwa wanafunzi 120 walioko Chuo Cha Maendeleo ya Wananchi Urambo(FDC) baada ya Mhe. Magret Sitta(MB) Jimbo la Urambo kutembelea kambi hiyo ya Umitashumita 2022 na kuchangia kiasi cha Tsh 1,000,000/= kwa ajili ya jezi na vifaa vingine vya michezo.
Mhe. Sitta ametoa pia mipira 10 ikiweno ya mpira wa miguu 6, mpira wa mikono 2 na netball 2 kwa lengo la kuhakikisha timu zote zinafanya mazoezi ya kutosha ili waienda Kanda na ngaz ya Taifa kuhakisha wanarudi na vikombe vya kutosha Urambo
"Michezo ni afya na michezo inachangamsha akili hasa kwenu ninyi watoto wadogo, mimi kama Mbunge wenu na mpenda michezo nimeona niungane nanyi ili kuhakikisha mnafanya mazoezi ya michezo mliyochaguliwa mkiwa na vifaa vya kutosha hivyo sisi tutabaki tunawaombee mkienda mrudi na vikombe, michezo oyeeee" amesema mhe. SittaAidha
Mhe. Sitta amewapa tena Tsh 60,000/= kwa ajili ya kupata soda kama pongezi kwa michezo mizuri walionyesha wanafunzi hao hii leo Julai 4, 2022
#SENSA2022: Jiandae Kuhesabiwa Tarehe 23 Agosti, 2022
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.