Mnamo tarehe 13.02.2025 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Paul Chacha alitembelea Miradi ya Afya Wilayani Urambo. Miradi iliyotembelewa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora ni kituo cha Afya katika Kata ya Vumilia pamoja na Kituo cha Afya katika Kata ya Songambele ambapo alitembelea Miradi hiyo ili kujionea maendeleo ya utekelezaji wa Miradi hiyo yenye zaidi ya Tsh. Milioni 950.
Katika Ziara hiyo Mhe. Paul Chacha aliweza kuambatana na Mkuu wa Wilaya ya Urambo Mhe. Dkt. Khamis Mkanachi aliyeambatana na baadhi ya Wajumbe wa kamati ya Usalama, Uongozi wa Chama cha Mapinduzi Wilayani Urambo Ukiwakilishwa na Katibu wa CCM Urambo Ndg. Himid Tweve, Wahe. Madiwani wa Kata za Vumilia na Songambele, Timu ya Wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Urambo wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Bi. Grace Quintine pamoja na Viongozi na Wataalamu mbalimbali.
Ziara hii ilikuwa Ziara ya Kawaida ya Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Tabora kwa ajili ya kukagua Miradi Mkoani hapa, ambapo alipongeza utekelezaji wa miradi hiyo huku akisisitiza umuhimu wa miradi hiyo ya afya kwa wananchi wa Wilaya ya Urambo.
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.