Taarifa za utekelezaji wa shughuli mbalimbali katika ngazi ya Kata za Wilaya ya Urambo zimeonyesha kuwa kwa kiasi kikubwa shughuli nyingi zimeweza kufanikiwa na changamoto zilizojitokeza ni chache.
Hayo yamebainika katika Mkutano wa Baraza la Madiwani la kujadili taarifa ya utekelezaji wa Shughuli za Serikali katika Robo ya Pili 2024/2025.
Mkutano huo ulioongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Mhe. Adam Malunkwi umefanyika tarehe 30.01.2025 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo na kuhudhuriwa na Wahe. Madiwani, Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, Wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Bw. Alex Marandu, Wawakilishi kutoka katika Taasisi za Umma, Watendaji wa Kata pamoja na wageni mbalimbali waalikwa.
Aidha katika Mkutano huo, imeelezwa kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo imefanikiwa kutekeleza miradi ya maendeleo katika kata mbalimbali kwa ajili ya kuhakikisha huduma bora zinawafikia wananchi.
Katika mkutano Huo Meneja wa Tabesco Wilaya ya Urambo amewaeleza Wahe. Madiwani kuwa, Changamoto kubwa inayoikumba shirika hilo ni pamoja na wizi wa nyaya za Earth ambazo husaidia kulinda transfoma, hivyo amewaasa kuwakumbusha wananchi wa maeneo hayo kulinda miundombinu ya umeme na kujiepusha na vitendo hivyo.
Aidha pamoja na mafanikio yaliyofikiwa changamoto mbalimbali zimeweza kuwasilishwa, pamoja na namna mbalimbali za utatuzi wake.
Ikumbukwe kuwa, Halmashauri ya Wilaya ya Urambo inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo, zikiwemo shule nne mpya ambapo shule mbili ni za Elimu ya awali na Msingi na Shule mbili ni kwa ajili ya Elimu ya Sekondari. Miradi hii inatekelezwa kupitia fedha kutoka Serikali kuu, Mapato ya ndani n.k
Kazi iendelee
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.