Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Bi. Grace Quintine amefanya kikao na Walimu Wakuu wa Shule za Sekondari, ambapo kikao hicho kimejikita katika Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo katika Sekta ya Elimu hasa katika ujenzi wa miundombinu kwa ajili ya shule hizo. Katika kikao hicho, Mkurugenzi Quintine amewaasa walimu wakuu waige mfano wa walimu wengine wanaotekeleza vyema miradi na kuhakikisha inakamilika katika viwango stahiki na kuhakikisha Fedha zinzotolewa zinafanya kazi kama ilivyoelekezwa na Serikali.
Aidha amesisitiza kuepuka ufujaji wa fedha hizo za miradi zinazotolewa ili kuwezesha miradi hiyo kukamilika kwa wakati na kwa viwango, kwani ufujaji wa fedha hizo hukwamisha juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha miundombinu ya Sekta ya Elimu inapatikana na kufikia jamii za Kitanzania. Mkurugenzi Mtendaji amesisitiza utendaji bora na ukamilishaji wa miradi katika mwaka ujao wa fedha na kusisitiza wenye miradi kuitekeleza vyema miradi hiyo.
Aidha Afisa Elimu pamoja na Afisa Tarafa wamesisitiza ushirikiano baina ya Walimu wakuu pamoja na viongozi wengine, na pindi inapotokea changamoto katika utekelezaji wa Miradi wasisite kuwasiliana na Mkurugenzi Mtendaji, Afisa Elimu na Watendaji wengine ili ziweze kushughulikiwa kwa wakati kwa maslahi ya Umma.
Katika hatua nyingine, Mkurugenzi Mtendaji amesisitiza matumizi ya mifumo ya Serikali hasa Mfumo wa manunuzi (Nest) kwani ni mfumo unaokidhi mahitaji ya Serikali pamoja na kupunguza gharama. Sambamba na hilo Afisa Manunuzi alipata wasaa wa kujibu maswali na kutoa maelekezo kwa Walimu wakuu juu ya Mfumo wa manunuzi (Nest) ambapo Walimu wakuu walikuwa na changamoto na kuuliza maswali ya Papo kwa hapo ili kufata maelekezo zaidi juu ya matumizi ya Mfumo huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Bi. Grace Quintine, amemshukuru Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi za Miradi hususan kwa sasa Fedha nyingi zimetolewa kwa ajili ya Ujenzi wa Shule Mpya, Umaliziaji wa Vyumba vya Madarasa, Matundu ya Vyoo kwa ajili ya Wanafunzi ili kuwawezesha kusoma vizuri.
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2024 Urambo . All rights reserved.