Kila ifikapo tarehe 09 ya Mwezi Disemba, Taifa linakumbuka Siku muhimu katika historia ya Tanzania Bara kwa namna ya kipekee kwani ndiyo siku ambayo Tanganyika ambayo ni Tanzania Bara ilipata Uhuru wake kutoka mikononi mwa Serikali ya Uingereza.
Hivyo kumekuwepo utamaduni wa kuiadhimisha siku hii Kwa kufanya matukio mbalimbali yanayotuleta pamoja. Katika kuadhimisha Miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara mwaka 2024, Wilaya ya Urambo imeadhimisha siku hii muhimu kwa kupanda Miti 200 katika Shule ya Msingi Azimio.
Zoezi hili limefanywa na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo kwa kushirikiana na Taasisi nyingine ikiwemo TK Movement wilayani Urambo.
Akizungumza katika tukio hilo, mgeni rasmi ambaye ni Ndg. James Kolugendo amesema kuwa miti hii italeta faida nyingi kwa watoto (Wanafunzi) pamoja na mazingira hapo baadae hivyo basi pamoja na kuadhimisha Siku ya Uhuru wa Tanzania Bara (Tanganyika) tumefanya pia jambo muhimu la utunzaji wa Mazingira.
Aidha, Katika hatua nyingine usafi wa mazingira waunganisha wananchi wa urambo katika maadhimisho ya miaka 63 ya uhuru wa tanzania bara.
Ambapo Katika muendelezo wa Shughuli za kijamii Wilayani Urambo, Wananchi, wafanyabiashara na watumishi wa Serikali wameungana na kufanya usafi katika Soko la ndizi ikiwa ni katika kuadhimisha Miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Aidha shughuli za Kijamii zimeendelea kuwaunganisha wananchi wa Urambo na zinatukumbusha Umoja na Mshikamano kama Taifa Moja bila kujali Jinsia, itikadi za Kisiasa, Dini n.k
Miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara:
"Uongozi Madhubuti na Ushirikishwaji wa Wananchi ni Msingi wa Maendeleo yetu"
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.