Halmashauri ya Wilaya ya Urambo imepokea fedha kwa ajili ya Utekelezaji wa Miradi 10 ya Elimu, fedha jumla ya Shilingi Bilioni 3.6
Miradi hii imeweza kutambulishwa katika kikao kazi kilichofanyika Tarehe 16 Julai, 2024 katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo na Kuhudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Urambo Dkt. Khamis A. Mkanachi (Mgeni Rasmi), Katibu Tawala wa Wilaya ya Urambo Ndg. Innocent Nsena, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Mhe. Adam Malunkwi, Afisa Usalama (W), Kamanda wa TAKUKURU (W), Mwenyekiti wa CCM Wilaya Ndg. Shabani Mussa, Katibu wa CCM Wilaya Ndg Himis Tweve, Mbunge wa Jimbo la Urambo Mhe. Margareth Sitta, Wahe. Madiwani wa Kata husika zenye Miradi, Wakuu wa Divisheni na Vitengo, Watendaji Kata na Maafisa Elimu Kata, Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji, Watendaji wa Vijiji, Waratibu wa Miradi pamoja na Maafisa Masuuli Wateule (Wakuu wa Shule)
Akizungumza Katika kikao kazi cha kutambulisha Miradi hiyo, Mhe Mkuu wa Wilaya ya Urambo Dkt. Khamis A. Mkanachi amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Bi. Grace Quintine kwa uwazi wake wa kushirikisha wadau mbalimbali kufahamu, kuandaa na utekelezaji wa Miradi hiyo, hatua ambayo itachangia ukamiliishwaji wa Miradi hiyo kwa wakati na kama ilivyokusudiwa.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo amemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa pongezi hizo. Aidha Bi. Quintine ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuleta fedha hizo kwa ajili ya Utekelezaji wa Miradi hiyo ambayo inaenda kuinua Sekta ya Elimu Wilayani Urambo.
Sambamba na Hilo amemshukuru na Kumpongeza Mbunge wa Jimbo la Urambo Mhe. Margareth Sitta kwa juhudi zake za dhati pamoja na ushirikiano wake na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji pamoja na jitihada za kufuatilia na kuhakikisha fedha za miradi hiyo zimepatikana.
Sambamba na Hilo Bi. Quintine amesisitiza Ukamilishaji wa Miradi ndani ya muda uliopangwa, kufuata utaratibu wa usimamizi wa Utekelezaji wa miradi hiyo pamoja na Ushirikiano baina ya Maafisa Masuuli wateule na Afisa Masuuli Mkuu (Mkurugenzi Mtendaji). Sambamba na Hilo Bi Quintine ametilia mkazo hoja ya Mhe. Dkt. Khamis A. Mkanachi ya kuweka mpango kamili kabla ya kuanza utekelezaji wa Miradi (Kujengea Mezani).
Hata hivyo Mkuu wa Wilaya ya Urambo Dkt. Mkanachi amesisitiza ushirikishwaji wa wananchi katika Miradi hiyo na kutumia wananchi kwa 20% kwa ajili ya nguvu kazi kwenye utekelezaji wa Miradi.
Miradi hiyo itatekelezwa katika Kata Nane za Halmashauri ya Wilaya ya Urambo ambapo kutakuwa na ujenzi wa mabweni na Shule mpya za Msingi na Sekondari zitakazojengwa mwaka huu.
Umaliziaji wa Bweni Shule ya Sekondari Urambo Day Kata ya Kiyungi gharama ya Mradi ni TSh. 136,123,769.92/= (EP4R)
Ujenzi wa Shule Mpya ya Msingi Katika Kata ya Kiyungi Gharama ya Mradi ni Tsh. 364,500,000/= (BOOST)
Ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari katika Kata ya Muungano gharama ya Mradi Tsh. 603,890,563.000/= (SEQUIP)
Ujenzi wa Mabweni Mawili katika Shule ya Sekondari Usoji Kata ya Songambele Gharama ya Mradi Tsh. 272,000,000/= (EP4R)
Ujenzi wa Nyumba ya Mwalimu Shule ya Sekondari Igunguli kata ya Uyogo Gharama ya Mradi ni Tsh. 110,000,000/= (SEQUIP)
Upanuzi wa Shule ya Sekondari Kasisi kuwa ya Kidato cha Tano na Sita (A-Level) Kata ya Kasisi gharama ya Mradi ni Tsh. 398,000,000/= (SEQUIP)
Ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari ya Kata ya Nsenda gharama ya Mradi ni Tsh. 603,890,563/= (SEQUIP)
Ujenzi wa Shule Mpya ya Msingi katika Kijiji cha Kamalendi Kata ya Ukondamoyo Gharama ya Mradi ni Tsh. 364,500,000/= (BOOST)
Upanuzi wa miundombinu ya Kidato cha 5 na 6 katika Shule ya Sekondari Uyumbu Kata ya Uyumbu Gharama ya Mradi ni Tsh. 398,000,000/= (SEQUIP)
Ujenzi wa Vyumba vitatu vya Madarasa, Mabweni 2, na vyoo Matundu 6 Katika Shule ya Sekondari Uyumbu kwa Ufadhili wa Barrick Gharama ya Mradi ni Tsh. 363,200,000/= (BARRICK)
Jumla ya Fedha zote zilizotolewa kwa ajili ya Miradi Mipya itakayoanza kutekelezwa mwaka huu ni Tsh. 3.614,194,895.92.
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2024 Urambo . All rights reserved.