• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Urambo  District  Council
Urambo  District  Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za mitaa Halmashauri ya wilaya ya Urambo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu msingi
      • Elimu sekondari
      • Idara ya Mazingira
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Fedha
    • Kata
      • Kata Zetu
    • Kibali cha Safari
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Watalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kiutumishi
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe. Madiwani
      • Mwaka 2020-2025
      • Mwaka 2015-2020
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Afya, Elimu na Maji
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya UKIMWI
      • Kamati Nyinginezo
        • Kamati ya Ugawaji wa Viwanja
        • Kamati ya Ajira
        • Kamati ya ALAT Mkoa
        • Wajumbe wa Mamlaka ya Mji Mdogo
    • Ratiba ya Vikao
    • Taarifa mbalimbali
  • Miradi
    • Miradi Mipya Itayotekelezwa
    • Miradi inayaoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
    • Sheria
    • Taarifa
    • Taratibu
    • Zabuni
  • Kituo cha Habari
    • Picha
    • Hotuba
    • Matukio
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video

URAMBO YATOA MILIONI 115.6 KWA VIKUNDI 8 VYA MIKOPO, MAMILIONI YANASUBIRI WENGINE.

Siku iliyowekwa: January 15th, 2025


Ikumbukwe Serikali ilisitisha utoaji wa Mikopo kwa ajili ya Wanawake, Vijana na watu wenye Ulemavu ili kuweka miongozo na kanuni madhubuti juu ya utoaji na urejeshaji wa mikopo hiyo.

Hata hivyo, Mnamo mwezi Julai, 2024 Serikali ilielekeza Muendelezo wa Utoaji wa Mikopo hiyo chini ya kanuni na Mwongozo wa utoaji Mikopo wa mwaka 2024.


Aidha baada ya usitishwaji wa utoaji wa mikopo Halmashauri ya Wilaya ya Urambo iliendelea kutenga fedha kwa ajili ya Makundi hayo kulingana na Mwongozo ambapo hadi kufunguliwa dirisha la Maombi Halmashauri ilikuwa imetenge zaidi ya Milioni 600.


Tarehe 14.01.2025 Mkuu wa Wilaya ya Urambo Mhe. Dkt. Khamis A. Mkanachi amekabidhi Mikopo yenye thamani ya Tsh. Milioni 115.6 kwa Vikundi mbalimbali Wilayani hapa (Milioni 85 kwa wanawake na 30,600,000/= kwa Vijana) ambavyo vinatoka katika kata za Urambo, Imalamakoye, Ussoke na Kapilula.

Katika Hafla hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Bi. Grace Quintine amevisistiza Vikundi hivyo kuzingatia biashara na marejesho ya wakati kwani lengo la Serikali ni kumuinua Kila mwananchi kiuchumi hivyo Mikopo hii isiyo na Riba inapaswa kutumika vyema na kurejeshwa kwa wakati ili kunufaisha Jamii ya Urambo.


Aidha Mgeni Rasmi Mhe. Dkt. Mkanachi amevieleza vikundi hivyo vikafanye biashara kulingana na walivyoomba ili pale watakapomaliza kurejesha waweze kuomba tena. Aidha Dkt. Mkanachi ameelekeza kuwa Vikundi vilivyokosa Sifa kwa awamu ya Kwanza viweze kuitwa ili kurekebisha makosa na kuelekezwa ili kutorudia makosa kama yaliyoonekana katika maombi yao ya awali ili waweze kuomba na kupata mikopo kwa awamu zijazo.


Aidha Mwenyekiti wa Halmashauri ya Urambo Mhe. Adam Malunkwi amemshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia kuendelea na mikopo hii huku akisisitiza vikundi vilivyopata mikopo kuwa wa mfano kwa vikundi vingine.


Nao wajasiriamali wamemshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwashika wajasiriamali mkono na kusema wamefarijika sana na wameahidi kutumia mikopo kama ilivyokusudiwa na kulipa kwa wakati ama ikiwezekana kabla ya wakati kwani wasipolipa kwa wakati wanazuia wanaotaka kupata wasiipate.


Kazi iendelee

Matangazo

  • Tangazo la nafasi za vijana za kujiunga na JKT 2024/2025 October 02, 2024
  • UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA AWAMU YA PILI May 01, 2025
  • Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili September 21, 2024
  • Tangazo kuhusu urejeshwaji wa mikopo ya vikundi vya vijana, wanawake na walemavu October 02, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MKURUGENZI MTENDAJI URAMBO ASHIRIKIANA NA MAAFISA KUCHANGIA VIFAA VYA WANAFUNZI WA UMITASHUMTA NA UMISSETA

    May 13, 2025
  • MHE. DKT. MKANACHI AZINDUA ZAHANATI YA KINHWA

    April 25, 2025
  • URAMBO YAADHIMISHA MUUNGANO KWA MATEMBEZI, USAFI NA KUPANDA MITI

    April 26, 2025
  • KAMATI YA FEDHA UONGOZI NA MIPANGO, YATEMBELEA KITUO CHA AFYA NA NYUMBA ZA WAKUU WA DIVISHENI

    April 25, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri wa maji, Prof. Makame Mbarawa
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Tovuti ya ofisi ya mkuu wa mkoa
  • FFARS USER GUIDE
  • PlanRep DOCUMENTATION
  • Facility Financial Accounting and Reporting System (FFARS)
  • Kata Zetu
  • BEMIS
  • Wahe. Madiwani

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa
  • Tovuti ya sekretarieti ya Ajira
  • Fomu ya Maadili ya Viongozi kwa Mtandao
  • Public Service
  • Matokeo ya Mtihani wa Taifa Tanzania.
  • Ikulu

Waliotembelea Tovuti

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Sehemu

Wasiliana nasi

    Bomani Urambo

    Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora

    Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824

    Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141

    Barua pepe: ded@urambodc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • sera ya faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.