Na Edward C Rumanyika
Wadau wa Elimu Urambo, wamekutana katika kikao cha kwanza kwa mwaka 2022 hii leo Februari 3, 2022 katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Urambo na kuazimia kwa pamoja kukomesha utoro shuleni kwa kuzitaka mamlaka zinazosimamia nidhamu ya wanafunzi wakiwemo walimu, wazazi, wenyeviti wa vijiji na vitongoji, watendaji wa kata na vijiji, mwanasheria wa Halmashauri, jeshi la polisi kuhakikisha swala la utoro shuleni linadhibitiwa ili mahudhurio yafike asilimia 100
Akizungumza na Wadau wa Elimu, mwenyekiti wa kikao hicho ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Urambo mhe. Louis Peter Bura amekemea baadhi ya tabia kwa watumishi, wazazi na walezi zinazoweza kupelekea kushuka kwa ufaulu wa wanafunzi na kupelekea wilaya kufanya vibaya katika matokeo ya mitihani ya ndani na ya Kitaifa.
Mhe. Bura amewataka Wadau wa Elimu hasa watendaji wa kata na vijiji kuweka kipaumbele na umuhimu wa kusimamia zoezi la upatikaji wa tofauri za akiba (benki ya matofari) katika kata na vijiji vyao kwa lengo la kusaidia ujenzi wa miradi ya elimu na afya kwa hatua za awali kabla ya serikali kumalizia hatua nyingine za ujenzi wa miradi hiyo, amesema anahamini ikiwa serikali za vijiji zitakuwa na tofari za kutosha na kuanzisha ujenzi wa madarasa kwa ajili ya kupunguza msungamo wa wanafunzi darasani, Halmashauri na serikali haitosita kuchangia fedha kwa ajili ya ukamilishaji wa miradi hiyo. Kwa msisitizo amekemea tabia ya baadhi ya watendaji wazembe wanaoshindwa kusimamia maazimio ya vikao vya maendeleo kwa kusema "mtumishi ambae analipwa na serikali na anaongozwa na mimi, kama huwezi kuendana na kasi yangu, Mkurugenzi yuko hapa sema atakupangia kazi nyingine".
Pia amewataka Wadau wa Elimu pamoja na wazazi kuhakisha watoto wanapata chakula cha mchana shuleni ili kupunguza utoro na kuwaongezea wanafunzi utulivu wa kuwasilikiza walimu wao pindi wanapokuwa darasani, amewaomba viongozi wa Kamati ya Maendeleo ya Kata kuhakikisha swala la chakula kwa wanafunzi shueni inakuwa ajenda ya kudumu katika mikutano yao.
Aidha, amekemea tabia ya baadhi ya watumishi hasa walimu kukopa zaidi ya uwezo wao wa mishahara jambo linalopelea kushindwa kutulia, kufundisha na kumaliza mitaala kwa wakati. Mhe. Bura amemtaka mkuu wa jeshi la polisi na TAKUKURU Urambo kubaini vikundi vinavyotoa mikopo bila utaratibu kwa kuweka riba kubwa na kuwatumia askali wa jeshi la polisi katika kurejesha mikopo hiyo kwa kuwanyang'anya watumishi kadi za benki na thamani mbalimbali za nyumbani.
Awali akisoma taarifa ya maendeleo ya elimu kwa Wadau wa Elimu, Katibu wa Mfuko wa Elimu ambae ni Afisa Elimu Sekondari wilaya ya Urambo Bi. Sara Nalogwa amesema hali ya ufaulu katika mitihani ya upimaji wa Kitaifa kwa mwaka 2021 umepanda kwa shule za msingi na sekondari. Kwa shule za msingi mwaka 2021 ufaulu Darasa la 7 ni asilimia 83.5 wakati mwaka 2020 ufaulu ulikuwa asilimia 81.4 na kwa shule za sekondari mwaka 2021 ufaulu ni asilimia 90.2 wakati mwaka 2020 ufaulu ilikuwa asilimia 88.5.
Akizungumza kwa niaba ya Wadau wa Elimu, mama mzazi Bi. Christina Ndituye wa mwanafunzi bora Dawasa Daudi Kawawa katika mtihani wa Taifa datasa la saba 2021 amewapongeza walimu wa shule ya msingi Songambele, Idara ya Elimu na viongozi wa Halmashauri kwa kumlea mtoto wake vizuri na kuweza kufaulu kwa kupata alama 279 kati ya 300 na kuwaomba Wadau wa Elimu Urambo kumwombea mwanae ili ndoto zake zikatimie na Mungu akijali arudi Urambo kuwatumikia wananchi na Taifa kwa ujumla.
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2024 Urambo . All rights reserved.