Kauli hiyo imetolewa na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Urambo Dkt. David Manyama, Mgeni Rasmi wa Maadhimisho ya Siku ya Wafamasia Duniani kwa ngazi ya Wilaya ya Urambo.
Dkt. David Manyama amewaeleza wafamasia waliojumuika pamoja katika maadhimisho hayo huku akiwaeleza kuwa Mfamasia ni mtu muhimu ambaye hukamilisha matibabu ya mgonjwa, kwani mfamasia hutoa maelekezo muhimu ya namna ya matumizi ya dawa alizopatiwa, hivyo endapo mfamasia hatompa maelekezo kamili mgonjwa ni ngumu mtu huyo kupona.
Aidha. Dkt. Manyama aliendelea kwa kuwapongeza kwa kuifanya siku ya Wafamasia ndani ya Wilaya ya Urambo kufana, na kuwaelekeza kuwa ni muhimu kwa wafamasia kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia sheria, kanuni na miongozo ya utoaji wa huduma kwa jamii ili kuwasaidia wananchi wanaofuata huduma ya Matibabu.
"Tunaamini kabisa, bila wafamasia kazi yetu inaishia katikati. Nyie ni kiungo kikubwa sana kati yetu sisi madaktari pamoja na wagonjwa na wateja. Nitumie nafasi hii kuwahitaji mfanye hizi kazi kwa weledi, muende mkafanye kazi kwa kufuata miongozo, taratibu na kanuni na maelezo yawe mazuri ili kuepuka madhara kwa mgonjwa au mteja" amesema Dkt. David Manyama.
Aidha Siku ya Wafamasia duniani imeadhimishwa tarehe 25.09.2025 ikisindikizwa na kauli mbiu isemayo "Ukifikiria Afya, Mfikirie Mfamasia", ambapo Wafamasia wa Wilaya ya Urambo wakiongoza na Mfamasia wa Wilaya Bw. Anthony Benard wameiadhimisha kwa matembezi ya pamoja na utoaji wa elimu kwa wananchi juu ya madhara ya matumizi holela ya dawa.
"Ukifikiria Afya, Mfikirie Mfamasia"
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.