Wajasiliamali Urambo wapata mkopo wa Tsh 114,683,000
Na Edward C Rumanyika
Katibu Tawala wa wilaya ya Urambo Ndg Paschal Byemelwa, kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Urambo amekabidhi vifaa na bidhaa mbalimbali zenye jumla ya thamani ya Tsh 114,683,000 kwa vikundi 9 vya wajasiliamali ambapo vikundi 4 ni wanawake na vikundi 5 ni vya vijana. Hafla hii imefanyika baada ya Mkutano wa kawaida wa baraza la Madiwani kwa kipindi cha robo ya 2 ya mwaka wa fedha 2021/2022. Vifaa hivyo ni pamoja na pikipiki 28 zenye thamani ya Tsh 72,800,000, bajaji 2 (gurudumu tatu) za kubebea mizigo zenye thamani ya Tsh 15,000,000, Urembo wa kutengeneza Mikoba, viatu, vikapu na pochi vyenye thamani ya Tsh 15,000,000, Mizinga 50 ya nyuki yenye thamani ya Tsh 3,610,000, vipuli vya mashine ya kusindika mafuta ya alizeti vyenye thamani ya Tsh 3,000,000, Bidhaa za kutengeneza sabuni na usindikaji wa nafaka thamani ya Tsh 5,273,000.
Ndg. Byemelwa ameipongeza Halmashauri ya wilaya ya Urambo kwa kuzingantia Sheria ya Fedha ya mwaka 2018 ya kuhakisha inatenga fedha asilimia 10 ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya mikopo ya vikundi vya wajasiliamali vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
Halikadhalika Ndg. Byemelwa amempongeza Mkurugenzi mtendaji na timu yake ya menejimenti kwa jitihada wanazozionyesha za ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maemdeleo na kusimamia vyema bajeti kwa kutenga asilimia 10 ya kila fedha inayokusanywa kwa mwaka wa fedha husika.
Amesisitiza "Nimefurahishwa na uamuzi wenu wahe madiwani wa kuwapatia vikundi hivi vitedea kazi badala fedha, kwa kufanya hivyo mmeisaidia serikali katika kupunguza tatizo la ajira maana nina imani kupitia vyombo hivi na vifaa hivi tayari mmetengeneza ajira kwa akina mama na vijana wetu wa urambo"
Awali akisoma taarifa ya ukopeshaji na urejeshaji wa mikopo inayotolewa na Halmashauri, Mkuu wa Idara ya maendeleo ya Jamii Ndg. Osear Mwabusila amesema kuna vikundi 3 vinastahili kupewa cheti cha pongezi kwa sababu vilifanya vizuri kwa kurejesha deni lao miezi miwili kabla ya muda wa marejesho kuisha, vikundi hivyo ni Motomoto Msengesi kata ya Uyumbu kijiji cha Msengesi, Mashujaa group kata ya Ukondamoyo kijiji cha Tumaini na Amka Investment kata ya Nsenda kijiji cha Itebulanda.
Akizungumza kwa niaba ya vikundi vilivyonufaika na mkopo huo, kiongozi wa kikundi cha Amka Investment Ndg. Simon Gabriel Ngayabosha kwa furaha kubwa ameshukuru Uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Urambo, serikali ya wamau ya sita na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kwa kuwaletea viongozi wenye maono na kuwaji wananchi kwani wanawasidia kupunguza umaskini na kuboresha maisha ya mtu mmoja mmoja na jami nzima kwa ujumla.
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.