Wananchi wa Kata ya Ugala Wilayani Urambo, wameonyesha furaha yao na kusema kuwa wameupokea mradi wa kituo kipya cha Afya katika Kata hiyo.
Wananchi hao wameonyesha furaha hiyo wakati ambao timu ya Wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Urambo iliyoongozwa na Mwakilishi wa Mkurugenzi Bw. Sadoki Magesa, ilipokwenda kutambulisha Mradi huo kwa wananchi pamoja na kutoa mafunzo kwa Kamati za utekelezaji wa mradi huo.
Aidha mradi wa ujenzi wa kituo kipya cha Afya katika kata ya Ugala, unatarajia kupokea fedha jumla ya Tsh. Milioni 500 kwa awamu mbili, ambapo kwa sasa Tsh. Milioni 250 zimeletwa na Serikali kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Mradi.
Akizungumza juu ya mradi huo, Diwani wa Kata ya Ugala Mhe. Lifa Sitta amesema kuwa, wamejiandaa vyema kuchangia nguvu kazi ili kuhakikisha mafanikio ya Mradi huo yanafikiwa na kurahisisha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi wa Kata ya Ugala.
Katika hatua nyingine,
UJENZI WA KITUO KIPYA KATA YA NSENDA UNAENDELEA KWA KASI
Hali ya ujenzi wa Kituo kipya cha Afya kata ya Nsenda Wilayani Urambo unaendelea kwa kasi, ikiwa ni siku chache tangu mradi huo utbulishwe kwa wananchi.
Mradi huo wenye thamani ya Tsh. 686,135,134, upo katika hatua ya Msingi na unatarajia kusaidia kwa kuokoa vifo vya wajawazito na watoto wachanga na malemgo mengine mengi.
Aidha, mradi wa ujenzi wa kituo cha Afya katika Kata ya Nsenda umekuja sambamba na mradi wa ujenzi wa kItuo kipya cha Afya katika kata ya Ugala, na kupelekea Wilaya ya Urambo kuwa na vituo 7 vya Afya.
Ikumbukwe kuwa, kupatikana kwa miradi hii ya Afya ni kutokana na juhudi za Mbunge Mhe. margaret Sitta pamoja na Serikali katika kuhakikisha Wananchi wanapata huduma bora za afya.
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.