"Ombi langu kwenu umuhimu wa wakinamama usibaki katika idadi kwa maana ya namba, hii idadi mkaigeuze ikalete matokeo na mabadiliko ambayo tunayoyataka"
Maneno haya yamezungumzwa na Mkuu wa Wilaya ya Urambo Mhe. Dkt Khamis Mkanachi ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika Kongano la Wanawake la kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake ngazi ya Wilaya.
Kongamano hilo limefanyika leo tarehe 04.03.2025 katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo ikiwa ni kuelekea katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake Ngazi ya Mkoa na Taifa tarehe 08.03.2025.
Katika Kongamano hilo lililogusa mada mbalimbali kama Afya ya Akili, Elimu ya Fedha na uchumi, Elimu kuhusu Saratani ya shingo ya kizazi/mji wa Uzazi, Lishe n.k wanawake na Wasichana wa Urambo walioshiriki waliweza kufaidika na mada hizo.
Aidha Mhe. Dkt. Mkanachi amewaeleza Wanawake kuwa katika maisha ya kila siku Wanawake na Wanaume wanategemeana na maumbile siyo udhaifu kwa namna yoyote ile.
Ikumbukwe kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Mara ya kwanza imeongozwa na Rais Bingwa na Kinara Mwanamke ambaye ni Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anayeiongoza vyema Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Serikali ya Awamu ya Sita
Aidha Jimbo la Urambo linawakilishwa na Mwanamke katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni Mhe. Margaret Sitta anayetetea na kuwasilisha hoja na changamoto mbalimbali kwa niaba ya Wananchi wa Urambo.
Sambamba na hilo, Halmashauri ya Wilaya ya Urambo inaye Mkurugenzi Mtendaji Kinara Mwanamke, anayeisimamia vyema na kuhakikisha Miradi na shughuli nyingine nyingi za Serikali zinatekelezwa katika kiwango cha Kuridhisha. Naye si Mwingine ni Bi. Grace Quintine.
Aidha katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Mwaka 2024, Urambo imepata Wenyeviti wa Vijiji pamoja na Vitongoji wanawake watakaoongoza na kusaidia jamii ya Wananchi wa Urambo. Hivyo basi, Urambo tunatambua, tunaheshimu na kuona kwa Macho mchango wa Mwanamke katika jamii kutoka Ngazi ya Taifa, Jimbo, Halmashauri ya Wilaya pamoja na Serikali za Vijiji na Vitongoji.
Aidha mapema hii leo Mbunge wa Jimbo la Urambo Mhe. Margareth Sitta ameongoza umati wa Wanawake wa Urambo katika Matembezi maalumu ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake ngazi ya Wilaya.
Matembezi hayo yamehusisha Wanawake kutoka Makundi mbalimbali Wilayani Urambo wakiwemo Viongozi wa Dini, Siasa, Vyama vya Wafanyakazi, wajasiriamali, Watumishi wa Umma kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Urambo n.k
Aidha umati huu wa Wanawake umefanya Matembezi kwa lengo la Kuelimisha na Kuikumbusha jamii juu ya umuhimu wa Mwanamke katika Jamii na umuhimu wa kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake kama Siku maalumu ya kutambua mchango wa Mwanamke katika Jamii.
"Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji"
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.