Mhe. Louis P. Bura Mkuu wa wilaya ya Urambo ameitaka jamii ya Urambo kuwathamini, kuwapenda na kuwajali walimu kwa kiwango cha juu sana kwa sababu walimu ndiyo wana muda mwingi wa kukaa na watoto wao na hivyo nafasi kubwa ya malezi ya watoto wanayo walimu, na kuwajali walimu itawaongezea morali ya ufundishaji na watoto watafanya vizuri kupitia mitihani ya ndani na ya Kitaifa hivyo kuongeza ufaulu wa wilaya.
Mhe. Bura amaeyasema hayo hii leo Septemba 27, 2022 kupitia hafla ya uzinduzi wa Mwongozo wa Elimu na Mikakati yake ngazi ya wilaya katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Urambo.
Mhe. Bura amewataka Wadau wa Maendeleo ya ELimu Urambo wakiwemo Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya, Wakuu wa Idara na Vitengo, Watendaji wa Kata, Waratibu Elimu Kata , Wakuu wa Shule na Walimu Wakuu kuutumia Mwongozo huu kuhakikisha malengo ya Taifa hasa mikakati iliyobainishwa inafikiwa kwa kutatua changamoto za elimu katika eneo lao bila kungojea viongozi wengine kwa lengo la kuhakikisha ufundishaji bora unafikiwa.
Mhe. Bura amewasihi Wadau wa Maendeleo ya Elimu Urambo kuacha kukata tamaa hasa wanapokutana na changamoto, "ni marukufuku kukata tamaa unapokutana na changamoto, kiongozi bora ni yule anaetatua changamoto na sisi tutafanya hiyo kazi kama tulivyokuwa tunafaya siku zote kwa ajili ya watu wa urambo, nasema siku zote wekeni mahusiano mazuri na jamii mkitaka kupunguza upungufu wa miundombinu katika shuke zetu " amesema Mhe. Bura.
Aidha, Mhe. Bura amewataka Wadau wa maendeleo ya Elimu Urambo kurejesha hali ya utendaji kazi kwa walimu kwa kuwasikiliza vizuri walimu na kubeba matatizo yao yote pindi wanapowasikiliza na kuwataka kutoa mrejesho wenye tija na kwa wakati. Kufanya hivyo kutawafanya walimu kutulia na kufundisha madarasani kuliko kutumia muda mwingi kuja Halmashauri kwa jambo ambalo lingetatuliwa huko huko kituoni.
Mhe. Bura amehitimisha kwa kuwaomba Wadau wa Maendeleo ya Elimu Urambo hasa Maafisa Elimu Kata kusimamia Mwongozo wa Elimu na Mikakati iliyotolewa bila kuupindisha na kuwataka ifikapo Oktoba 1, 2022 Mwongozo huu uwe wazi na bayana kwa walimu wote maana wao ndiyo kiungo cha Afisa Elimu wilaya na walimu wetu.
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.