Kitengo cha ugavi
Halmashauri ya Wilaya Urambo
Halmashauri ya Wilaya ya Urambo ina kitengo cha ugavi ambacho kumeundwa kwa mujibu wa sheria ya manunuzi na 7 ya mwaka 2011 kufugu na 37 ambapo sheria hiyo inaitaka taasisi ya serikali iwe na kiktengo cha ugavi (Procurement Management Unit –PMU).
Kitengo cha ugavi kinakiwa kiwe na mkuu wa kitengo mwenye elimu aliyosomea ujuzi huo na sifa, uzoefu katika kazi za manununzi na pia awe amesajiriwa na Bodi ya manunuzi (Procurement Professional Body).
Kwa mujibu wa sheria mkuu wa kitengo cha ugavi ataripoti moja kwa moja Afisa masuhuli wa taasisi husika.
Afisa masuhuri wa taasisi atahakikisha kwamba kitengo cha ugavi (PMU) kinatengewa fedha kwenye bajeti ili kiweze kutimiza majukumu yake.
Kitengo cha ugavi kinasimamia manunuzi yote toka idara na vitengo vilivyoko kwenye Halmashauri kitengo hiki kina wataalamu ambao wanafanya kazi kwa mujibu wa sheria ya manunuzi.
Aidha kitengo cha ugavi mbali na kufanyakazi na idara na vitengo vya Halmashauri, pia kinafanya kazi kwa karibu sana kwa kushirikiana na Bodi ya Zabuni ya Halmashauri ambayo majukumu yake yameainishwa na sheria ya manunuzi na 7 ya mwaka 2011 kifungu cha 33 (1) (a) –( e).
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.