FURSA ZA UWEKEZAJI KATIKA MAZAO –WILAYA YA URAMBO.
UTANGULIZI.
Wilaya ya Urambo ina jumla ya hekta 87,984 zinazofaa kwa kilimo, kati ya hizo hekta 10,400 zinafaa kwa kilimo cha Umwagiliaji eneo hili ni sawa na 11.8% ya eneo linalofaa kwa kilimo. Kati ya eneo linalofaa kwa kilimo ni hekta zisizozidi 59,000 ndiyo zinazolimwa sawa na 67%. Hivyo kaya za wakulima Wilayani Urambo zina wastani wa ekari 2 kwa ajili ya kilimo. Wilaya ya Urambo hupata mvua kiasi cha mm 600 hadi mm 1,200 kwa mwaka.
Hali ya hewa, udongo na mazingira Urambo inaruhusu ustawishaji mzuri wa mazao ya biashara kama Tumbaku, karanga, alizeti, pamba na korosho. Mazao ya chakula ni mahindi, mpunga, viazi vitamu na mhogo.
|
FURSA ZA KIBIASHARA KATIKA MAZAO
A. RASLIMALI ZINAZOWEZESHA KUWEKEZA KIWANDA CHA TUMBAKU
WATU: Kuna kaya za wakulima 30,700 kati ya kaya zote 35,024.
Idadi ya watu ambao ni wakulima ni 64,000 kati ya watu 225,664
Idadi ya wakulima wa tumbaku kutoka kwenye Vyama Vya Msingi (AMCOS) 55 ni 10,642
ARDHI: Eneo linalofaa kwa kilimo ni Hekta 87,984 kati ya eneo lote la wilaya lenye Hekta 611,000.
ENEO LA UJENZI WA KIWANDA:
Kuna eneo la Hekta 32 lililotengwa, kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha tumbaku
MIUNDO MBINU ILIYOPO ENEO LA KIWANDA:
UZALISHAJI WA TUMBAKU: Wilaya ya Urambo inao uwezo wa kuzalisha zaidi ya kilo 15,000,000 kwa mwaka, kwa kutumia Vyama vya Msingi (AMCOS) 55 vilivyopo Urambo
KWANI KIWANDA URAMBO:
Kiwanda cha tumbaku kikijengwa Urambo, kutokana na kuwa eneo la katikati kwa ushirikishwaji, kinaweza kuchakata tumbaku kutoka Vyama Vikuu Vya Ushirika vya:
MAMBO YA KUFANYA KABLA YA UWEKEZAJI WA KIWANDA CHA TUMBAKU URAMBO
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.