Mnamo tarehe 28.01.2025 Ulifanyika Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi, likiwa na lengo kuu la kupitia rasimu ya mpango wa Bajeti wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026.
Katika kikao hicho Baraza la wafanyakazi liliweza kutoa mapendekezo mbalimbali yenye nia ya kuboresha rasimu hiyo yenye bajeti ya zaidi ya Tsh. Bilioni 33 ili iweze kukidhi mahitaji ya Halmashauri ya Wilaya ya Urambo.
Mkutano wa Baraza hilo ulitembelewa na Mkuu wa Wilaya ya Urambo Mhe. Dkt. Khamis A Mkanachi ambaye amepongeza jitihada za baraza hilo huku akisema kuwa amejifunza jambo katika Baraza hilo, misingi yake na majukumu yake.
Aidha Kikao cha Baraza la Wafanyakazi kiliongozwa na Mwenyekiti wake Bi. Grace Quintine ambaye alipendekeza baadhi ya majina kwa ajili ya uchaguzi wa Katibu na Katibu msaidizi wa baraza hilo. Ambapo ulifanyika uchaguzi na Bw. Fabian kuibuka mshindi na kuwa Katibu wa Baraza hilo, huku Bi. Elizabeth Makoye akifuata kwa kura na kuwa Katibu Msaidizi.
Ikumbukwe kuwa, Halmashauri ya Wilaya ya Urambo inaendelea na mchakato wa kupitisha rasimu ya mpango wa Bajeti yake ya 2025/2026 katika vikao vyote vya kisheria ili iweze kupitishwa na kuwasilishwa katika ngazi za juu zaidi.
Kazi iendelee
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.