Urambo, Tabora.
Wakuu wa divisheni na vitengo vya Halmashauri ya Wilaya ya Urambo, tarehe 06.10.2025 wamefanya ziara ya kutembelea maeneo tarajiwa ya Uwekezaji na ujenzi wa Miradi ya maendeleo yenye zaidi ya ekari 85 katika kata za Ussoke, Kapilula na Urambo.
Ziara hiyo iliyoongozwa na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Bw. Alex Marandu ililenga kubaini na kutazama maeneo hayo yaliyotengwa ili kutumia vyema fursa zilizopo na kuinua pato la Halmashauri.
Aidha Bw. Marandu amesisitiza Watendaji wa Kata kuendelea kutenga maeneo mengi zaidi makubwa kwa ajili ya uhakika wa Upatikanaji wake pale maeneo hayo yatakapohitajika iwe ni kwa ajili ya kuwekeza au ujenzi wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo.
Katika ziara hiyo, CMT iliweza kutembelea maeneo mbalimbali ikiwemo eneo la St. Vincent ambapo Jengo jipya la Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji linatarajia kujengwa kuanzia mwaka huu wa fedha (2025/2026).
Aidha katika ziara hiyo wakuu wa idara walitembelea sehemu maalumu iliyotengwa kwa ajili ya kuhifadhia taka ngumu na laini, ambapo waliweza pia kutoa ushauri wa kuliwezesha dampo hilo liwe katika ubora kulingana na bajeti ya Halmashauri iliyowekwa.
Pamoja na kuwaonesha maeneo hayo ya uwekezaji na ujenzi wa Miradi ya maendeleo, Afisa Ardhi Wilaya ya Urambo Bw. Ernest Mwakang'ata, aliweza kuwaeleza Wajumbe wa CMT kuwa, Halmashauri ya Wilaya ya Urambo bado inayo nafasi ya kuwekeza zaidi kupitia maeneo yaliyopo, hivyo Halmashauri isisite kuendelea kutenga maeneo zaidi kwa ajili ya shughuli hizo za Miradi ya maendeleo na uwekezaji.
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.