Urambo - Tabora.
Wananchi wa Kijiji cha Muungano kilichopo katika Kata ya Muungano Wilayani Urambo, wameridhishwa na ufafanuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Bi. Grace Quintine, juu ya mchanganuo wa fedha zilizotoka kwa Mkandarasi wa ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR).
Bi. Grace Quintine ambaye kwa mujibu wa sheria ndiye msimamizi wa mapato katika Halmashauri ya Wilaya, ametoa ufafanuzi huo katika kikao kilichofanyika terehe 10.06.2025 zilipo ofisi ya kijiji hicho, baada ya wananchi hao kuhitaji ufafanuzi wa manufaa ya kijiji juu ya fedha zinazopatikana kutokana na shughuli za mkandarasi katika kijiji hicho.
Aidha, baada ya kutoa ufafanuzi juu ya mchanganuo wa fedha zitakazopatikana kutoka kwa mkandarasi na kuwaeleza kuwa kijiji kina wajibu wa kueleza Halmashauri ya Wilaya kipaumbele chao ili fedha zitakazopatikana ziweze kutumika, aidha Bi. Grace Quintine alieleza pia kuhusu wajibu wa mkandarasi kwa jamii anapofanyia kazi.
Hata hivyo Bi. Quintine amewapongeza viongozi wa kata hiyo akiwemo Diwani wa Kata hiyo kwa Ushirikiano wake wakati wa ufuatiliaji wa fedha hizo ili ziwe zinaingia kwenye kijiji na hatimaye sasa kijiji hicho kunufaika na mradi huo.
Ikumbukwe kuwa, kijiji cha Muungano ni moja kati ya vijiji vinavyotoa madini ya ujenzi kupitia mlima, kwa ajili ya ujenzi wa Reli ya kisasa kutoka Tabora - Kigoma, kipande cha Urambo.
Aidha, kwa upande wa wananchi wa Kijiji hicho, wameridhishwa na ufafanuzi uliotolewa na Mkurugenzi Mtendaji na kushukuru kwa Miradi inayoendelea kutekelezwa katika kata hiyo, ambapo kwa mwaka huu wa fedha wamepata shule mpya ya sekondari na wanatarajia Kituo cha Afya siku za usoni.
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.