Bi. Grace Quintine Mkurugenzi Mtendaji(W) Urambo ameipongeza Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamamii na Huduma za Lishe kwa ufuatiliaji na usimamiaji wa lishe kwa mama wajawazito baada ya mafanikio makubwa ya utoaji wa huduma ya vidonge vya madini ya chuma na asidi ya foliki kuongezeka kutoka asilimia 97 robo ya tatu kufikia asilimia 99.1 robo ya nne kwa mwaka ulioshia 30 Juni,2023.
Bi Quntine amefurahishwa na ushirikishwaji wa wadau wa Kamati ya Lishe kwa kuhusisha asasi za kiraia na madhehebu ya dini na kusema muunganiko huo uwe chachu ya kuhakikisha elimu ya lishe bora inatolewa katika mikusanyiko ya watu kuanzia shuleni, makanisani, misikitini, semina na washa za asasi za kiraia ili jamii ya ya Urambo inakuwa imara na yenye afya nzuri.
Bi. Quintine ameitaka divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma ya Lishe kutenga dawati la Elimu ya Lishe Bora kila kituo cha kutolea huduma kwa akina mama wajawazito wanaohudhuria kliniki ili wajengewe uwezo wa jinsi ya kukaa na kumshikilia mtoto wakati wa kumnyonyesha na pia namna ya kuandaa chakula chenye lishe bora kwa ajili ya familia zao ili kutokomeza utapiamlo.
Akisoma taarifa ya robo ya nne ya mwaka 2022/2023 Bi. Chonge Mazengo Afisa Lishe wa Wilaya kupitia kikao cha Kamati ya Lishe kilichoketi Juali 21, 2023 katika ukumbi mdogo wa mikutano wa Halmashauri amesema hadi kufikia 30 Juni, 2023 jumla ya akina mama wajawazito 10,912 kati ya 11,010 waliudhuria kliniki na kupatiwa vidonge vya madini ya chuma na asidi ya foliki.
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2024 Urambo . All rights reserved.