Halmashauri ya Wilaya ya Urambo imepokea pongezi kwa kupata hati safi, usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo pamoja na kukusanya vyema mapato ya Halmashauri kutoka katika vyanzo mbalimbali.
Pongezi hizo zimetolewa katika mkutano maalum wa Baraza la Halmashauri la kujadili taarifa ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Urambo imepata hati safi.
Akizungumza katika mkutano huo, Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora Dkt. John Mboya amesema kuwa, pamoja na kupata hati safi, Tukumbuke kuwa Serikali katika miaka minne ya Uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan imeleta fedha nyingi zaidi ya Bilioni 40 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali katika ngazi ya Halmashauri kwa ajili ya kuwanufaisha wananchi wa Urambo.
Aidha ameendelea kwa kusema kuwa Halmashauri imefanya vizuri utekelezaji wa miradi hiyo na katika kukusanya mapato kwani hadi kufikia Tarehe 31.05.2025 Halmashauri iliweza kufikisha makusanyo ya asilimia 97 (97%) ambao ni wastani mzuri.
Akizungumzia makusanyo ya mapato, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Mhe. Adam Malunkwi ameongeza kwa kusema kuwa, asilimia zilizobaki kwa ajili ya kufikia lengo ni chache na zinaweza kufikika. Hivyo amempongeza Mkurugenzi Mtendaji na Wataalamu kwa jitihada zao za kukusanya mapato ya Halmashauri bila kuchoka, kwa manufaa ya wananchi wa Urambo.
Ikumbukwe kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo ilipanga kukusanya jumla ya Tsh. Bilioni 3.8 Na kufikia tarehe 31.05.2025 kilikusanywa jumla ya kiasi cha Tsh. Bilioni 3.6 Sawa na asilimia hizo 97.
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.