Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango (FUM) wakiongozwa na Mhe. Adam Malunkwi Mwenyekiti(W) Urambo wakiambatana na Mkurugenzi Mtendaji(W) Urambo pamoja na Timu ya Wataalamu, Alhamisi ya leo 9 Novemba, 2023 wamefanya ziara ya kutembelea, kukagua na kutoa maelekezo kwa jumla ya miradi 7 inayoendelea kutekelezwa katika maeneo tofauti ndani ya halmashauri ya wilaya ya Urambo.
Kamati ya FUM, wameweza kutembelea mradi wa umaliziaji wa ujenzi wa kituo cha Afya Usske Mlimani kata ya Uyumbu, ujenzi wa zahanati ya Kinhwa kata ya Kiloleni, mradi wa SEQUIP ujenzi wa nyumba za walimu (two in one) Kasisi shule ya sekondari kata ya Kasisi, umaliziaji wa ujenzi wa kituo cha Afya Songambele, ujenzi wa zahanati ya Ukwanga, ujenzi wa bweni Usoji sekondari kata ya Songambele na mradi wa SEQUIP ujenzi wa Igunguli sekondari kata ya Uyogo.
Pamoja na kuwa Kamati ya FUM imeridhishwa na hatua mbalimbali ya utekelezaji wa miradi hiyo imeweza pia kutoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mtendaji(W) ya kuhakikisha anaelekeza raslimali fedha kwenye miradi hiyo kulingana na bajeti, kuongeza kasi ya ujenzi na usimamizi wa karibu ili miradi ikamilike kwa wakati na itumike kwa malengo yaliyokusudiwa
Aidha kamati ya FUM iliweza pia kutembelea mradi wa ujenzi wa kituo cha Polisi kata ya Songambele na ujenzi upo katika hatua ya ukamilishaji.
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.