Halmashauri ya Wilaya ya Urambo imefanya tafrija ya kuwaaga Waheshimiwa Madiwani waliofikia ukomo wa Uongozi wao wakiwa kama wawakilishi wa Wananchi wa Wilaya ya Urambo.
Madiwani hao waliohudumu kwa kipimdi cha miaka mitano, wameagwa mbele ya Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Urambo, Uongozi wa Chama cha Mapinduzi, Mbunge wa Jimbo la Urambo pamoja na Wakuu wa Divisheni na Vitengo vya Halmashauri ya Wilaya ya Urambo.
Katika tafrija hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Bi. Grace Quintine amewatakia kheri katika Mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa 2025 ili waweze kurejea wote wakiwa salama, pia amewaahidi kuwa wataikuta Halmashauri ya Wilaya ya Urambo ikiwa salama, kwani yote yatakayofanyika yataenda sambamba na Bajeti ambayo waliipitisha.
Bi. Grace Quintine ameendelea kwa kusema kuwa, miradi yote ambayo inatekelezwa na iliyopokelewa mwishoni mwa mwaka wa fedha 2024/2025 itakamilishwa kama ambavyo imekusudiwa.
Aidha, amemtakia kheri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Mbunge wa Jimbo la Urambo Mhe. Margaret Sitta katika mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa 2025.
"Urambo, Familia Moja"
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.