• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Urambo  District  Council
Urambo  District  Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za mitaa Halmashauri ya wilaya ya Urambo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu msingi
      • Elimu sekondari
      • Idara ya Mazingira
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Fedha
    • Kata
      • Kata Zetu
    • Kibali cha Safari
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Watalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kiutumishi
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe. Madiwani
      • Mwaka 2020-2025
      • Mwaka 2015-2020
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Afya, Elimu na Maji
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya UKIMWI
      • Kamati Nyinginezo
        • Kamati ya Ugawaji wa Viwanja
        • Kamati ya Ajira
        • Kamati ya ALAT Mkoa
        • Wajumbe wa Mamlaka ya Mji Mdogo
    • Ratiba ya Vikao
    • Taarifa mbalimbali
  • Miradi
    • Miradi Mipya Itayotekelezwa
    • Miradi inayaoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
    • Sheria
    • Taarifa
    • Taratibu
    • Zabuni
  • Kituo cha Habari
    • Picha
    • Hotuba
    • Matukio
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video

MAMA SAMIA AMEGUSA MAISHA YA WANAURAMBO KWA NISHATI SAFI

Siku iliyowekwa: January 17th, 2025

Mkuu wa Wilaya ya Urambo Mhe. Dkt. Khamis Mkanachi amezindua zoezi la utoaji wa Gesi za Ruzuku kwa wananchi Wilayani Urambo tarehe 16.01.2025.


Gesi hizi za Ruzuku zimeletwa chini ya Mpango wa Nishati Safi unaotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kushirikiana na kampuni ya gesi ya Oryx Energies, mpango wenye lengo la kuhakikisha wananchi wanahama kutoka katika matumizi ya Kuni na Mkaa hadi matumizi ya gesi.


Hatua hii madhubuti imesaidia kupunguza athari za hewa chafu (Carbon dioxide) ambayo ni chanzo cha maradhi mbalimbali kwa binadamu hivyo matumizi ya gesi yatasaidia pia katika utunzaji wa Mazingira kwa kupunguza ukataji wa miti kwa ajili ya kuni na Mkaa.


Akizungumza katika Uzinduzi wa Kampeni hiyo, Dkt. Mkanachi amesema, "Nyote ni mashahidi Mama Samia anaendelea kuyagusa maisha yetu kwenye kila hatua, mmeona kwenye mikopo ya Halmashauri imetolewa Shilingi milioni 115 kupitia vikundi 8. Na zimebaki fedha kama Milioni 593,843,365 zimebaki zinasubiri Quater (robo) ya pili vikundi vingine vipewe, vipo vikundi 45, na tumeelekeza mtu wa maendeleo ya jamii na timu yake akakae na vikundi vyote arekebishe kasoro zilizopo kwenye documents (nyaraka) zao na wote waweze kukopesheka. Tunapokwenda kwenye awamu ya pili ya mikopo, fedha yote  itoke iende kwa wananchi, ndivyo Mama Samia anavyotaka, kuwawezesha wananchi wake kiuchumi"


Ameendelea kusema "Mtakumbuka Novemba 2022 Mhe. Rais alizindua mkakati wa matumizi ya nishati safi na amejipambanua kuwa kinara wa nishati mbadala kwa Afrika na kuwakomboa kinamama.


Mama Samia amekusudia kuwasaidia kinamama. Mmeelezwa Mtungi huu una thamani ya Tsh. 55,000/= ukienda kuununua dukani, Mama Samia kwa mapenzi aliyonayo na kwa kuchampion Ajenda ya matumizi ya nishati safi ambayo ni mkakati uliowekwa na Serikali kufikia mwaka 2030 anataka asilimia 80 ya Watanzania Wote wawe majumbani kwao wawe wanatumia nishati safi, nishati ya Gesi. Tunaondokana na kuni, tunaondokana na Mkaa ndiyo lengo la Mama Samia"


Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Bi. Grace Quintine ameshukuru kwa niaba ya Wananchi na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo na kusema kuwa anaamini wananchi wa Urambo wapo tayari na gesi hazitosalia kwani wote wameonyesha nyuso za Furaha kwani Serikali imepunguza Tsh 35,000 na kuwezesha majiko ya Gesi kupatikana kwa Tsh 20,000. Hivyo wananchi wakaeleze wengine ili sote tuhamie katika matumizi ya nishati safi.


Aidha akizungumza katika hafla hiyo Mwakilishi wa kampuni ya Oryx Energies kwa mikoa ya Kigoma na Tabora Bw. Gibson amesema kuwa Wilaya ya Urambo imetengewa majiko 3,255, hivyo kuhakikisha majiko haya yanafika kwa wananchi. Amesema vigezo vya kupata majiko haya ni Namba ya NIDA kwa jiko moja pamoja na Tsh. 20,000. Hivyo utapatiwa Jiko pamoja na elimu ya matumizi ya gesi hiyo.


Aidha Wananchi wa Urambo watapata fursa za kuwa mawakala wa kampuni ya Oryx Energies ili kusaidia wananchi kujaza gesi pale zitakapowaishia.

Matangazo

  • Tangazo la nafasi za vijana za kujiunga na JKT 2024/2025 October 02, 2024
  • UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA AWAMU YA PILI May 01, 2025
  • Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili September 21, 2024
  • Tangazo kuhusu urejeshwaji wa mikopo ya vikundi vya vijana, wanawake na walemavu October 02, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MKURUGENZI MTENDAJI URAMBO ASHIRIKIANA NA MAAFISA KUCHANGIA VIFAA VYA WANAFUNZI WA UMITASHUMTA NA UMISSETA

    May 13, 2025
  • MHE. DKT. MKANACHI AZINDUA ZAHANATI YA KINHWA

    April 25, 2025
  • URAMBO YAADHIMISHA MUUNGANO KWA MATEMBEZI, USAFI NA KUPANDA MITI

    April 26, 2025
  • KAMATI YA FEDHA UONGOZI NA MIPANGO, YATEMBELEA KITUO CHA AFYA NA NYUMBA ZA WAKUU WA DIVISHENI

    April 25, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri wa maji, Prof. Makame Mbarawa
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Tovuti ya ofisi ya mkuu wa mkoa
  • FFARS USER GUIDE
  • PlanRep DOCUMENTATION
  • Facility Financial Accounting and Reporting System (FFARS)
  • Kata Zetu
  • BEMIS
  • Wahe. Madiwani

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa
  • Tovuti ya sekretarieti ya Ajira
  • Fomu ya Maadili ya Viongozi kwa Mtandao
  • Public Service
  • Matokeo ya Mtihani wa Taifa Tanzania.
  • Ikulu

Waliotembelea Tovuti

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Sehemu

Wasiliana nasi

    Bomani Urambo

    Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora

    Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824

    Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141

    Barua pepe: ded@urambodc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • sera ya faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.